Ticker

6/recent/ticker-posts

TANESCO YAONGEZA JITIHADA KUKAKABILIANA NA UPUNGUFU WA UMEME



**********************

Na Magrethy Katengu

Shirika la Umeme TANESCO limendelea kufanya juhudi za kukabiliana na changamoto ya umeme kwa kukamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa LM6000 katika kituo cha Ubungo namba III na umeshaanza kuingiza megawati 35 za umeme katika Gridi ya Taifa.

Akizungumza na Waandishu ew habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme TANESCO Mhandisi Maharage Chande TANESCO amesema jitihada hizo zilianza kuanzia 25 Novemba 2022 kama ilivyoekezwa hapo awali

" Tayari tumeshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kidatu na umeshaanza kuzalisha megawati 50 za umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia 30 Novemba 2022;Matengenezo ya mtambo mmoja katika kituo cha Kinyerezi namba II yameshakamilika na tayari umeshaanza kuzalisha megawati 215 za umeme kuanzia tarehe 24 Novemba 2022"amesema Chande

Hata hivyo amesema majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea hivyo kwa sasa mitambo hii inaingiza jumla ya megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa na jitihada zinazoendelea mategemeo yake ni hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba 2022, mitambo hii itakuwa inazalisha jumla ya megawati 90.

Sanjari na hayo bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba III ambapo baada ya kukamilika mwishoni mwa Disemba 2022, itazalisha jumla ya megawati 40 za umeme.

"Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanya kazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa. Iwapo mvua zitaendelea kunyesha katika mabwawa yote ya kufua umeme na matengenezo yaliyobakia kukamilika kama yalivyopangwa, basi tunategemea hali ya umeme itaendelea kuimarika "amesema Chande

Sanjari na hayo amesema na hivyo wanatarajia kiasi cha upungufu wa umeme kwa siku kuendelea kupungua kutoka wastani wa kati ya megawati 300 hadi 350 wiki iliyopita hadi kufikia megawati 215 za umeme wiki hii huku kazi zote zikiendelea kufanyika, Shirika litaendelea kutoa taarifa ya hali ya umeme na ratiba ya upungufu wa umeme kadri inavyozidi kuimarika .

Post a Comment

0 Comments