Ticker

6/recent/ticker-posts

TCRA YAKUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imekutana na watoa huduma za mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha sekta ya mawasiliano.

Mkutano huo wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa umefanyika leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza ambapo washiriki wa mkutano pia wamepewa Elimu kuhusu matumizi ya Mfumo wa Tanzanite.

Akitoa ufafanuzi wa Hoja za wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa yatokanayo na kikao cha wadau cha tarehe 24 Mei,2022 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema TCRA imekuwa ikifanya mapitio ya kanuni zinazosimamia sekta ya mawasiliano mara kwa mara na hivi sasa mapitio ya kanuni yanaendelea ambapo Ada zimeshuka kwa kiasi kikubwa lakini pia imefanya mikutano ya kisekta mara kwa mara hasa kunapokuwa na suala linalohitaji ushirikishwaji wa wadau.

"TCRA itaendelea kufanya mikutano hii kwa ajili ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano hapa nchini na kuhusu Sifa za waajiriwa kwenye sekta ya utangazaji, TCRA inaelekeza wamilki wa vyombo vya habari wazingatie sheria, kanuni na miongozo ya ajira iliyopo. Pia Suala la Taaluma kwa waandishi ni la kisera",amesema.

Akizungumzia kuhusu madai ya Utaratibu wa kila kituo cha radio kuwa cha kibiashara (Commercial category) haufai kwamba Redio nyingine ni za kihuduma zaidi, kama vile kueneza dini na masuala mengine ya kijamii Kuziweka kwenye kundi moja na zile za Kibiashara si jambo jema, Mihayo amesema Mgawanyo wa leseni umewekwa kwa kuzingatia makundi mbalimbali ya huduma kwa wananchi. TCRA inashauri wanaoomba kutoa huduma wachague kundi stahiki kutoka na huduma wanayotaka kuitoa.

Kuhusu Ombi la Kuwe na utekelezaji huduma za kamati ya maudhui kwenye ofisi za kanda ili kupunguza gharama kwa wanaohitajika kutokea kwenye kamati hiyo kutoka Mikoa nje ya Dar es Salaam, amesema TCRA imekuwa ikiandaa vikao vya kamati ya maudhui Kanda kutegemeana na malalamiko yalikotokea ili kuondoa usumbufu na gharama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

"Kwa upande wa Mrejesho wa haraka kutoka TCRA kwenda kwa watoa huduma kwa masuala mbalimbali. Dawati la huduma lipo kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya wadau,piga namba 0800008272 bure. TCRA inasaidiaje kukomeshwa kwa jumbe zenye udanganyifu (mf. Tuma pesa kwenye namba hii).Elimu inaendelea kutolewa kwa watumiaji wa huduma kuwa makini wakati wa utumiaji wa huduma. Aidha Mamlaka ya Mawasiliano imetoa namba maalum 15040 kwa ajili ya kupokea taarifa za kiutapeli na kuzishughulikia",ameongeza Mihayo.

Kwa upande wa Changamoto ya udukuzi kwenye Online media. Mwenye leseni analindwaje na TCRA?, Mhandisi Mihayo amesema TCRA inatoa elimu kwa umma wa matumizi sahihi na salama ya mitandao ikiwemo namna ya kujilinda na masuala ya udukuzi. Aidha, Mmiliki wa kituo husika analo jukumu la kuweka ulinzi wa kutosha kwenye mtandao wake kwa kuweka uthibitisho wa hatua takribani mbili (Two Factor Authentication) kujilinda na udukuzi wa akaunti kwenye online media.

Aidha TCRA inawashauri waandishi wa habari kuhakikisha wanafikia vigezo vinavyotakiwa na sheria ya habari ili kuleta ubunifu, ufanisi na tija katika sekta ya habari na utangazaji.

Kuhusu malalamiko ya Umeme kwamba sio wa uhakika maeneo mengi hali inayosababisga kuongeza gharama za urushaji wa Matangazo, TCRA inawashauri wamilki wa vyombao vya habari kuweka miundombinu ya nishati mbadala ya uhakika na gharama nafuu ili kukabiliana na changamoto hiyo.

"Kuhusu Umoja wa mafundi simu unao wataalam wenye ujuzi wa kushughulikia changamoto mbalimbali za kiufundi. Utaratibu wa kuwatambua mafundi simu, kuweka kumbukumbu zao na kuwajea uwezo unaendelea ili kuboresha ufanisi wao. Lakini pia TCRA kwa kushirikiana na wadau wa mazingira ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata taka za kielektroniki ili kuondoa athari za kimazingira zinazoweza kuletwa na uwepo wa taka hizo",ameeleza.

Aidha TCRA itaendelea kuboresha mifumo yake ikiwemo Mfumo Tanzanite Portal ili kurahishisha utoaji wa huduma kwa wadau pamoja na kuwapunguzi gharama za upatikanaji wa huduma.

"Ni kwa namna gani vionjo (teaser) sahihi vya habari vitumike kupunguza upotoshaji. Hususani kwenye eneo la TV za mtandaoni na mitandao ya Youtube?. TCRA inawahimiza kuzingatia sheria, kanuni na weledi katika kuandaa na kutoa habari kwa kutumia mifumo yote husika. TCRA itaendelea kufanya mikutano ya kisekta kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa taratibu",amesema.

"Kuhusu Ombi la Wamiliki wa Cable TV waruhusiwe kutengeneza maudhui ya ndani. Matumizi ya mkongo wa Taifa ni gharama kubwa. TCRA/serikali iweze kutoa ruzuku kwa muda mfupi ili kupunguza gharama kwa mtoa huduma. Leseni wanazopewa watoa huduma wa cable ni kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kuwezesha huduma za Tv kuwafikia watumiaji. Na kama wanataka kutoa huduma ya kutengeneza maudhui ya channel moja ya sasa basi waombe leseni husika kutoka TCRA",ameongeza.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza
Mtaalamu wa TEHAMA kutoka TCRA, Ibrahim Ibrahim akitoa elimu kuhusu Mfumo wa Tanzanite kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumatano Desemba 7,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza

Mhandisi mwandamizi wa TCRA Kadaya Baluhye  akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa

Post a Comment

0 Comments