Baadhi ya wadau wa habari kutoka nchi 15 wakiwa kwenye warsha ya siku tatu wakijadili itifaki ya usimamizi wa habari na mazingira.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufungua warsha ya Siku tatu kwa wadau wa Bahari leo Desemba 12 jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 12
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
**************************
NA Magrethy Katengu
Imeelezwa kuwa Ili kusaidia mazingira ya na maji bahari yanatuzwa vizuri wadau wa mazingira kutoka nchi mwanachama 15 wa Afrika wameshiriki katika Warsha ya siku tatu kwa ajili ya kukuza uelewa wa pamoja juu ya Mkataba wa kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari.
Haya ameyasema leo Jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi wakati akifungua warsha ya siku tatu ya iliyohudhuriwa na wadau wa ndani ikiwemo Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa meli Tanzania (TASAC),Bandari,Taasisi ya Bahari ya Dar es salaam(DMI)na wawakilishi Nchi 14 zinazotumia usafiri maji Afrika ikiwa na lengo kujadiliana namna kuipa kipaumbele mkataba wa kimataifa kwaajili ya kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha viumbe vitakavyo zaliwa majini vinakuwa hai udhibiti viumbe vamizi .
"Hali ya bahari Mazingira ya Bahari kwa sasa ni manzuri lakini tahadhari mbalimbali lazima zitolewa kwa ajili ya vizazi vya vijavyo kwani ifahamike kuwa vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia sera ya uchumi wa bluu, sasa bahari inapochafuka na inapoharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa bluu inakuwa ngumu kwani kwa sababu ya viumbe ambavyo vinasababisha uchumi vitapotea"amesema Possi
Akizungumza kuhusiana na vyombo vya usafiri wa majini amesema navyo vinasababisha uharibifu wa mazingira kwani kutokana maji wanayoveba kutoka sehemu moja kwenda nyingine Ili kuleta usawa wa Usafirishaji mizigo wanaposhusha wanatakiwa kwenda kuyamwaga katikati ya bahari siyo kumwaga holela ili kuepuka viumbe vamizi hivyo kupitia warsha hiyo itatilia mkazo wa uridhiaji wa itifaki ya sheria ya bahari kwa ajili ya kuendeleza uelewa mpana wa wadau wote.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Abdi Mkeyenge amesema Shirika hilo limekasimiwa mamlaka ya kudhibiti mazingira ya majini na Maji yanayotokana na uchafunzi mazingira ya viumbe vya maji unaosababishwa na vyombo vya Usafiri Majini hivyo madhumuni ya warsha hiyo ni uelewa wa pamoja wa Jinsi ya kudhibiti uchafuzi wa maji, kusimamia masuala ya usafiri majini.
Hata hivyo Mkurugenzi amesema maji yanayowekwa kwenye meli Ili kuleta usawa wa kukaa sana yale yale maji yakishushwa yanaweza kuzalisha viumbe wengine ambavyo vitakuwa hatarishi kwa uendelevu viumbe ambao wapo baharini na tunavihitaji lazima kuwepo na sera ya Meli baada ya kushusha mizigo ikamwage maji katikati ya bahari au Ili kuepuka uvamizi wa viumbe hatarishi kwa viumbe vilivyopo
"Uchumi wa bluu unaweza usifikiwe kama maji yanakuwa hayadhibitiwi. Kwahiyo hatutaufikia uchumi wa bluu kama mikataba hii hatutairidhia na kuzingatia ni jinsi gani tunaweza kujikinga na hivyo viumbe ambavyo vinaweza kuzalishwa hivyo warsha hii itakuja na majibu nmna ya kudhibiti mazingira ya majini"amesema Abdi
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo amesema kuwa maji yanahobebwa na meli yanasaidia meli pale ambapo inakuwa haina mzigo pia ikiwa na mzigo mdogo yanapunguzwa au kuongezwa ili kuweka uzito sawa katika meli na Maji hayo watu wenye meli wamekuwa wakiyamwaga baharini jambo ambalo sio zuri.
"Maji hayo yanaviumbe na mimea ambayo sio asili ya huku kwetu kwa hiyo ikitokea yanamwagwa baharini yatakuwa na viumbe wavamizi wataleta namna tofauti ya kimazingira Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) liliona umhimu wa kuweza kudhibiti hali hiyo kwa sababu kimazingira sio sawa, kinachotakiwa ni kuto kumwagwa baharini kama nchi mwanachama wa IMO tunatakiwa kuridhia mkataba huo ili kuweza kusimamia kuwa haitakiwi ukifika bandarini kumwaga maji inatakiwa kwenda kumwagwa katika kati ya habari ili yasiweze kuleta shida katika eneo letu la mazingira ya maji.
Amesema Kwa Tanzania Sasaivi tupo katika hali nzuri kwa sababu tumeshaanza kuridhia mkataba pia amesema Kama wizara wameshatoa maoni na mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na mkataba huu. Na mpaka sasa wameshaanza kupokea maoni yao
Shirika la Kimataifa la Bahati linatoa Elimu kwa Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya bahari hivyo wananchi wanachama nchi 14 Afrika wameshiriki katika warsha hiyo ili kupata uwelewa wa pamoja na kutengezena Mkataba wa pamoja utakaoridhiwa na kanuni zitakazotumika
0 Comments