Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKANDARASI WATAHADHARISHWA KUFUATA MATAKWA YA MIKATABA YAO.

Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa mkataba wa mradi REA III.katika hafla ya makabidhiano mkataba wa mradi wa Rea III kwa Mkoa wa Tanga ambao zaidi ya sh bilioni 11 zitagarimu katika mradi huo ambao utatekelezwa katika Wilaya 6 kati ya 8 za Mkoa huo.
Mkurugenzi mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy akizungumza na wajumbe na wakandarasi wa mkutano wa makabidhiano mkataba wa mradi wa Rea III kwa Mkoa wa Tanga ambao zaidi ya sh bilioni 11 zitagarimu katika mradi huo ambao utatekelezwa katika Wilaya 6 kati ya 8 za Mkoa huo.

Wajumbe wa mkutano wakifuatilia kwa ukaribu.hafla ya kusaini na kukabidhiana mkataba wa mradi wa Rea III kwa Mkoa wa Tanga ambao zaidi ya sh bilioni 11 zitagarimu katika mradi huo ambao utatekelezwa katika Wilaya 6 kati ya 8 za Mkoa huo..

Mgurugenzi akiongea na mkuu wa Kaimu mkuu wa Mkoa ofini kwake kabla ya kufanya makabidhiano, katikati kushoto ni kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tanga Willium Masomwe.


*************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MKURUGENZI mkuu Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Hassan Saidy amesema hawatajihusisha kubeba majukumu ya Mkandarasi ambaye atatekeleza mradi wake kinyume na makubaliano ya mkataba waliosaini kati yao.


Mhandisi huyo ameyasema hayo kabla ya kuwekeana saini na kukabidhiana mkataba wa mradi wa Rea III kwa Mkoa wa Tanga ambao zaidi ya sh bilioni 11 zitagarimu katika mradi huo ambao utatekelezwa katika Wilaya 6 kati ya 8 za Mkoa huo.


Aidha amebainisha kwamba moja ya makubaliano ya mkataba kati ya REA na Mkandarasi ni kutumia rasirimali watu na vitu ndani ya eneo linalotekelezwa mradi lakini pia kuhakikisha wanatumia vifaa vyenye ubora ili kuondokana na kero ya kukataliwa katika utekelezaji wao.


"Hakikisheni kwanza kandarasi wote wanafanya kazi zao kulingana na mikataba, kwenye kazi ambazo hazihitaji utaalamu tumieni vijana wa eneo husika kufanya kazi hizo, lakini pia hakikisheni mnapofanya nao kazi muwalipe kwa wakati" amebainisha.


"Hatutalipia fedha kwa vifaa vya ujenzi visivyo na ubora lakini pia tunasisitiza kufanya kazi kwa kushirikiana, hakikisheni kwamba mkifanya kazi mnawashirikisha wenyeji na viongozi wa eneo husika" amesisitiza.


Naye Kaimu mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa amesema serikali imedhamitia kujenga uchumi wa nchi na mtu mmo mmoja kwa kuendelea kujenga miradi mbalimbali ambayo unatoa ajira kwa vijana lakini pia wakina mama.


"Fedha za mradi huu ni sh bilioni 79 zilizotolewa kwa nchi nzima kutekeleza REA III, na tumepata bahati ya kuletewa kiasi cha zaidi ya sh bilioni 11, mradi huu tumepewa utekelezaji wa miezi 18 hadi kukamilika, tuendelee kusisitiza kwamba iwe hivyo hivyo kusiwe na mabadiliko yoyote" amesema Mgandilwa.


Mgandilwa ametoa tahadhari kwa viongozi na wananchi, kwamba kwa yeyote atakayejaribu kutaka kuharibu miundombinu kwa njia moja au nyingine hatua kali zitachukuliwa kwani atakuwa hana nia njema na serikali kwa kuhujumu uchumi wa nchi.


"Kumekuwa na baadhi ya wananchi wana tabia ya kuharibu miundombinu, sasa kama mtaharibu itakuwa ni ngumu kwa serikali kutimiza malengo yake, na pia wapo baadhi ya viongozi wa siasa ambapo huku jambo linafanyika vingine yeye atakwenda kutoa kauli tofauti kwa wananchi, niwaombe, mtunze miundombinu mnayoletewa kwani ni kwa faida yenu na vizazi vyenu vijavyo" amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments