Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU AAGIZA HOSPITALI YA KATAVI IANZE KUTOA HUDUMA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya maabara wakati alipokagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Katavi, Disemba 12, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Patrice Sarafine (kulia) kuhusu ujenzi wa Hospitali hiyo iliyopo Mpanda, Disemba 12,2022. Waziri Mkuu alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi akiwa katika ziara ya kikazi ya Mkoa wa Katavi, Disemba 12, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Patrice Sarafine kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi iliyopo Mpanda, Disemba 12,2022. Waziri Mkuu alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Patrice Sarafine kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi iliyopo Mpanda mjini, Disemba 12,2022. Waziri Mkuu alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkkuu)

Muonekano majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya Mkoa wa Katavi, Disemba 12, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*********************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Patrice Serafin ahakikishe ifikapo Januari Mosi , 2023 hospitali hiyo iwe imeanza kutoa huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuu Kassim ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Disemba 12, 2022) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo inatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 12.4 itakapokamilika na imefikia asilimia 92 ya ujenzi.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Katavi kuhakikisha ifikapo Disemba 23, 2022 awe amefikisha huduma ya umeme katika hospitali hiyo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutawezesha kulaza wagonjwa 170 na hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia imeanza kuweka huduma ya kipimo cha CT-SCAN katika hospitali zote za mikoa. “Kwa mara ya kwanza Katavi watapata huduma ya kipimo cha CT-SCAN katika hospitali hii.”

Naye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amedhamiria kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

“Dhamira hii njema ya Rais Dkt. Samia tunaiona na ndio maana hapa manispaa ya Mpanda kunajengwa vituo vya afya vitano na vipo katika hatua ya umaliziaji, pia ametoa shilingi milioni 150 kwa ajili ujenzi wa zahanati”

Post a Comment

0 Comments