Ticker

6/recent/ticker-posts

JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI YAADHIMISHA MIAKA 46 YA CCM KWA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO


Viongozi wa CCM wakiangalia majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 

Na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog
Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imeadhimisha Miaka 46 ya CCM kwa kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Wafanyabiashara wa Mitumba la Ngokolo Mitumbani na ujenzi wa Mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.


Mbali ya kutembelea miradi hiyo pia wamepanda miti katika shule hiyo sambamba na kuzungumza na wananchi katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Ijumaa Januari 27,2023, Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa shule na soko la Ngokolo Mitumbani.

Siagi amesema Jumuiya ya Wazazi CCM inaridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi ya Soko la Ngokolo Mitumbani pamoja na shule ya sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Shinyanga.


“Tunaipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa namna mnavyotekeleza Ilani ya CCM, Mhe. Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, Waheshimiwa Madiwani, viongozi wa Chama pamoja na viongozi na wananchi kwa ushirikiano mnaotoa kufanikisha ujenzi wa miradi. Kwa namna ya pekee tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga”,amesema Siagi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi akizungumza leo Ijumaa Januari 27,2023 kwenye Soko la Ngokolo Mitumbani

Siagi amewataka viongozi wa CCM kutembelea ofisi za kata na halmashauri ili kupata takwimu kwa ajili ya kuzungumzia miradi inayotekelezwa pamoja na kutenga muda kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu kuja kutatua kero za wananchi.

“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, viongozi tusiwe sehemu ya kero, tukawa watu wa kulalamika tu badala ya kutatua kero za wananchi, kama jambo lipo ngazi ya tawi litatuliwe kwenye ngazi ya tawi badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu kuja kutatua”,amesema Siagi.

“Pia naomba tuendeleze umoja na mshikamano wetu, uchaguzi umeisha sasa ni wakati wa kufanya kazi. Kila aliye na dhamana ya uongozi tumpe nafasi aongoze. Napenda tuwe wamoja ili tutekeleze tuliyopanga, sitavumilia migogoro, kama upo kwenye chama unatukwamisha hatutakuvumilia”,amesema Siagi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi (katikati) akishiriki ujenzi wa Soko la Kisasa la Ngokolo Mitumbani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Anord Makombe amewataka wananchi kuendelea kuiamini CCM kwani inafanya mambo makubwa yanayoonekana huku akisisitiza kuwa hawana wasiwasi na mikutano ya hadhara kwani Serikali ya CCM imetekeleza miradi mikubwa inayonufaisha wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mlindoko amesema CCM ina kila sababu za kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kutoa kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Mlindoko ametumia fursa hiyo kulinda watoto ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa watoto ikiwemo kubakwa na kulawitiwa.

“Naomba tuungane kulaani na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwafichua wahalifu wanaoharibu watoto wetu, watoto wanafanyia vitendo viovu,Sasa hivi maadili yameharibika, watoto wanabakwa na wanalawitiwa,mbaya zaidi wazazi wanapokea pesa kesi zinamalizwa kienyeji”, ameongeza Mlindoko.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi amehamasisha jamii kupeleka watoto shule badala ya kuwaozesha huku akieleza kuwa CCM itafanya ziara ya kuwasaka watoto waliopewa mimba na kuachishwa masomo na kuwabaini wahalifu.

“Ni wajibu wa mzazi kupeleka shule, na ni lazima tuwachunge watoto wetu kwani hivi sasa kuna wimbi la vijana mashoga. Mzazi usimwamini mtu yeyote na kumuachia mtoto wako kwa sababu vitendo vya ukatili wa kijinsia vinafanywa na ndugu wa karibu kabisa”,amesema Kibabi.

“Tuwachunge watoto wetu na tuwakanye kujiingiza kwenye mambo ya ajabu. Wazazi mnachangia kuharibu watoto, utakuta mzazi anamtaka binti yake amletee chips, kuku wakati mtoto hana kazi, unamfanya mtoto aanze kudanga matokeo yake anapata maambukizi ya magonjwa au anazalishwa unakuwa wa kulea watoto tu. Ili familia yako iwe salama peleka mtoto shule, aelimike kwa ajili ya maisha yake”,ameongeza Kibabi.
Ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani kata ya Ngokolo ukiendelea.

Akizungumzia ujenzi wa Mradi wa Soko la Ngokolo Mitumbani, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha ujenzi ulianza Novemba 1,2022 na unatarajiwa kukamilika Februari 28,2023 ukigharimu shilingi Milioni 480 zinazotokana na mapato ya ndani ambapo wafanyabiashara wa mitumba zaidi ya 200 watanufaika na mradi huo .

Tesha amesema pia wanajenga choo cha kisasa kitakachogharimu shilingi Milioni 38 na kwamba baada ya ujenzi wa soko hilo litakalokuwa na vinne wataongeza tena vibanda vingine vinne vitakavyotumika kwa wafanyabiashara ambao hawakuwa kwenye eneo hilo la Ngokolo Mitumbani ili kuhakikisha wafanyabiashara wote wa mitumba wanahamia kwenye soko hilo litakalofanya kazi usiku na mchana.

Naye Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Cleophace Mzungu akielezea kuhusu ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga, amesema Manispaa ya Shinyanga ilipokea shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na unatekelezwa kwa kutumia Force Account.
Muonekano wa majengo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga.

“Majengo yanayojengwa na hatua zilizofikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa 12 ambapo vyumba 6 vyenye ofisi viko katika hatua za ukamilishaji, pia vyumba 2 vyenye vyoo, na vyumba 4 vipo katika hatua ya ukamilishaji. Kazi zilizokwisha fanyika ni kujenga msingi,kuinua kuta,kuezeka,kupiga lipu,kupiga dari,kufanya skiming, kupiga rangi kwa baadhi ya vyumba. Bado kuwekwa milango,madirisha,sakafu,upigaji rangi na samani kwa baadhi ya vyumba. Kazi ya ukamishaji inaendelea”,ameeleza Mzungu.

“Maabara za Fizikia, Jiografia, Kemia na Biolojia pia vimejengwa na kuezekwa na kupigwa lipu,kazi ya kupaua pia imekamilika, vyumba vya maabara vimewekwa dari,kazi ya kukamilisha ndani inaendelea ikiwa ni pamoja na kuweka vigae,rangi na mifumo ya maji,umeme na gesi”,amesema.
Muonekano wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 

“Vyoo vya matundu 16 vimejengwa na kupigwa lipu,kuwekewa vigae na kazi nyingine kama mfumo wa maji safi na maji taka na kukamilisha mifumo ya umeme. Mabweni matano pia yamejengwa na yameezekwa,bweni moja linakamilishwa.Kazi inayoendelea ni kuweka vigae, uchimbaji wa shimo la kutengeneza mfumo wa gesi (Bio Gas) kutokana na maji taka za binadamu unaendelea, bado kuweka mfumo wa umeme na maji”,ameeleza.

Amesema ujenzi wa bwalo na jengo la utawala unaendelea na nyumba 2 za walimu zimejengwa na zipo katika hatua ya ukamilishaji na kazi zingine zinazotarajiwa kufanyika ni kutengeneza viwanja vya michezo,kupanda miti na kuchonga samani za ndani.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi akizungumza leo Ijumaa Januari 27,2023 kwenye Soko la Ngokolo Mitumbani ambapo ujenzi wake unaendelea. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani kata ya Ngokolo ukiendelea
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi na viongozi mbalimbali wa CCM wakitembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Ngokolo Mitumbani
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi na viongozi mbalimbali wa CCM wakitembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Ngokolo Mitumbani
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi (kulia) na viongozi mbalimbali wa CCM wakishiriki ujenzi wa Soko la Kisasa la Ngokolo Mitumbani
Viongozi mbalimbali wa CCM wakishiriki ujenzi wa Soko la Kisasa la Ngokolo Mitumbani
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Diwani wa kata ya Ngokolo, Victor Mkwizu akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi  akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Katibu wa Siasa na Uenezi  CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mlindoko akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Ngokolo Mitumbani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ikitembelea na kukagua ujenzi wa Mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya CCM.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Cleophace Mzungu  akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Cleophace Mzungu akionesha viongozi wa CCM majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakati Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ikiadhimisha miaka 46 ya CCM.
Viongozi wa CCM wakitembelea majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Cleophace Mzungu akionesha viongozi wa CCM majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakiangalia majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Cleophace Mzungu akionesha viongozi wa CCM majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakitembelea majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakitembelea majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakiwa kwenye majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakiangalia majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakiangalia majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Muonekano wa majengo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Muonekano wa majengo yanayoendelea kujengwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga  
Muonekano wa majengo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakipanda miti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakipanda miti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakipanda miti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Viongozi wa CCM wakipanda miti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa Siasa na Uenezi  CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mlindoko akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Robert Elisha akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Wanachama wa CCM na wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Post a Comment

0 Comments