Ticker

6/recent/ticker-posts

MAJAMBAZI WANNE WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM***********************

Na Magrethy Katengu

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu wanne Januari 8 mwaka huu majira ya saa 6;30 mchana eneo la Mabibo External Ubungo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 9, 2023 jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne Muliro amesema majambazi hao kuwa ni pamoja na Athuman Yusuph Mbalilo @Soti (50) Mkazi wa Kimara Temboni, na Mpoki Raphael @ Mwangwisya (41) mkazi wa Mbezi luis.

ACP Muliro amesema wawili wanashikiliwa kwa tuhuma nzito za kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora pesa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

“Ukamataji huo ulitokana na taarifa fiche ya kuwepo kwa kundi hilo la kihalifu ambalo lilionekana kuanza kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha kuanzia tarehe 01/01/ 2023 hadi tarehe 07/1/2023 katika Jiji la Dar es Salaam,” amesema ACP Muliro

Hata hivyo Watuhumiwa hao wanne walikutana kupanga na kujiandaa kufanya uhalifu na walipobaini kuzingirwa na askari Polisi mmoja wao alitoa bastola yake na kupiga risasi kuwashambulia askari katika mazingira hayo askari haraka walijihami na kuwajeruhi watuhumiwa wote wanne kwa risasi na kufanikiwa kuwakamata .

ACP Muliro ameeleza kwamba mahojiano ya awali na watuhumiwa hao na kumbukumbu za kihalifu za Polisi zimeonesha kuwa miongoni mwao waliwahi kukamatwa na kukaa kwenye mahabusu ya Keko kwa tuhuma za mauaji na unyanganyi na walitoka 2017 na mmoja wao akakimbilia nchi jirani na alirudi 2022 na kushiriki matukio yakiwemo jaribio la uporaji eneo la Mtaa wa Tandamti Kariakoo, kupora pesa huku wakitishia bunduki eneo la Kunduchi Mtongani, Goba walitishia silaha na kupora pesa, Keko na Vikindu Wilaya ya Mkuranga .

“Watuhumiwa hawa baada ya kukamatwa waliweza kuwaonesha askari bunduki aina ya AK 47 yenye namba za usajili UC 3889 1998 ikiwa na risasi 24 ndani ya Magazine, Bastola moja aina Star iliyofutwa namba ikiwa na Risasi nne (4) ndani ya magazini na zilikamatwa pia Pikipiki mbili aina ya Boxer nyeusi, MC 665 DMD na MC 475 DPH ambazoz zikitumiwa kwenda na kutoka kwenye maeneo ya matukio yaliyotajwa,” ameeleza ACP Muliro.

ACP Muliro ameongeza kwa kusema kutokana na majeraha waliyoyapata wakati askari wakijihami kwa risasi wahalifu hao walipata majeraha na wamepelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu lakini hali zao sio nzuri wanaendelea na matibabu watakapopona watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili

"Juhudi za kuwatafuta majambazi wengine ambao hawajakamatwa zinaendelea na lazima watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria Jeshi letu liko imara linafanya kazi usiku na mchana hivyo tunahakikisha wananchi wanafanya shughuli zao za kiuchumi Kwa amani na usalama "amesema Muliro

Aidha Jeshi la Polisi linachukizwa sana na halitavumilia hata kidogo kuona wahalifu wakiwasumbua wananchi kwa vitendo vya kihalifu.Jeshi halitakuwa na huruma lakini litazingatia sheria kuwashughulikia kwa haraka sana kila atakaye jihusisha au kutenda vitendo vya ovyo vya kihalifu

Kwa upande wake Mhanga aliyenusurika na Majambazi hayo Fortinatusi John Mkazi wa Madale amesema yeye shughuli zake za kibiashara anafanyia Goba hivyo alivamiwa na Majambazi hayo wakiwa na silaha za moto hivyo aliamuru wateja wake walale chini huku vijana wake wa ulinzi wakijibizana nao na silaha na kuwashinda hivyo hawakufanikiwa kuchukua chochote walikumbia kutokana na Ofisi yake kuna mfumo wa kamera walitoa taarifa Kwa Jeshi la Polisi hivyo video yote ya wahalifu ilionekana na kuchukuliwa na kwa Kuwa Jeshi la Polisi chini Kamanda Muliro liko imara waliwatafita Majambazi hayo na kuyakamata na kutuita hivyo tumeshuhudia begi walilokuja nalo na silaha walizumia ni zenyewe hivyo tunashukuru sana kwa jitihada zao

Naye Jospaki Mwasimoto Mkazi wa Halmashauri ya Kinondoni Tanki bovu Amesema yeye akiwa katika shughuli zake Maeneo ya alivamiwa na Majambazi hayo na kuanza kumkaba na kutaka fedha ndipo walipofanikiwa kuchukua kiasi Cha milioni tatu na kumjeruhi kupelekea kulazwa

Post a Comment

0 Comments