Ticker

6/recent/ticker-posts

MSAKO KWA WANAFUNZI UMEANZA SASA, HAKIKISHANI WOTE WANAJIUNGA KIDATO CHA KWANZA" RC CHALAMILA.***********************

Na Shemsa Mussa. KAGERA.


Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert John Chalamila leo amezungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na udahili kwa wanafunzi.


Amesema kwa mwaka 2023 wanafunzi waliohitajika kujiunga kidato cha kwanza ni 59175 na mpaka sasa wanafunzi waliojiunga ni 35526 sawa na asilimia 60 huku wilaya ya Biharamlo ikiwa na asilimia 45 pekee za wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza.


"Nasikitika kuona wilaya yangu ya biharamlo kuwa ya mwisho kuripoti wanafunzi kidoto cha kwanza tatizo litajulikana na kutatuliwa " amesema Chalamila.


Aidha amesema kuwa msako wa kuwasaka wanafunzi wanaotakiwa kujiunga kidato cha kwanza umeanza lasmi majumbani na kuwagiza wakuu wa wilaya kusimamia kazi hiyo pia amewaonya wazazi wanaowaficha watoto kwa lengo la kulima na kufanya kazi za nyumbani bila kwenda shule ukibainika hatua kali zitahusika juu yake.

"Kuna baadhi ya wazazi wanawapeleka watoto wao mashambani kulima na msimu ukiisha wanawapeleka shule huku wakiwa na vizingizio kibao sasa jiandaeni kufuata sheria"amesema Chalamila.


Hata hivyo amewasisitiza wazazi kuona umuhimu wa chakula shuleni kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa bidii na kuongeza ufahuru bila njaa na kusema kuwa ni marufuku waalimu wakuu kuwachangisha wazazi chakula cha mwaka mzima na kusema kuwa ni vema kuchanjia taratibu bila kumsumbua mzazi na kwaiyari yao sio lazima ila ni vema mzazi kuona umuhimu wa suala hilo.


Pia amesema kwa awamu ya kwanda ndani ya Mkoa kagera yalijengwa jumla ya madarasa 881 na awamu ya pili yamejegwa 514 nia na lengo la ujenzi wa madarasa hayo ni mategemeo ya kuwa na wanafunzi wengi.

Post a Comment

0 Comments