Ticker

6/recent/ticker-posts

TUSIUHARIBU MWAKA KWA SIKU MOJA-RC CHALAMILA.**********
Na Shemsa Mussa, KAGERA.


Mkuu wa Mkoa kagera mhe Albert John Chalamila amewataka wanachi wa Mkoa huo kusherehekea vizuri Sikukuu ya Mwaka mpya kwa amani na utulivu.

Amesema hayo pindi akizungumza na wananchi kupitia Waandishi wa habari walipokutana Ofisini kwake kwa lengo la kuwatakia sikukuu njema wananchi wa mkoa kagera na taifa kwa ujumla .


"Nawatakieni sikukuu njema wananchi wote wa mkoa ila ninawasihi sherehekeeni kwa amani bila kufanya vurugu za aina yoyote " amesema Chalamila.


Aidha amewasisitiza wananchi kutumia mkesha wa mwaka mpya kwenda katika nyumba za ibada na kumuomba Mungu zaidi kuliko kutumia siku hiyo kufanya uasherati(Uzinzi ) ama vitendo vibaya kwani kufanya hivyo ni kuendelea kujitia mikosi na kuutia mkoa nuksi .


"Utumie mkesha kwenda kanisani ,msikitini sio kumbi za staree fanyeni vitendo vya kuubariki mkoa na sio nuksi na laana " amesema Chalamila.


Hata hivyo amesema baada ya sikukuu ya mwaka kazi zinaendelea za kuukuza mkoa na uendelevu wa utekelezaji wa miradi , na kumalizi kwa kumshukuru rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazofanya kwa wananchi wake.

Post a Comment

0 Comments