Ticker

6/recent/ticker-posts

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM KATA YA BUGURUNI WATEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI KWENYE KATA HIYO


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Buguruni pamoja na Viongozi wa CCM wa kata hiyo leo Januari 30,2023 wametembelea miradi inayotekelezwa na Serikali kwa ilani ya Chama hicho ambapo wametembelea miradi ya ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari, mradi wa ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua pamoja na mradi wa ufyatuaji wa matofali wa kikundi cha Wajane (MAHAME) ambao wamekopeshwa mkopo kutokana na fedha zinazotolewa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Buguruni Bw. Mwishehe Rajabu amesema asilimia 10 kutoka halmashauri, asilimia 4 zimegawiwa katika kikundi cha MAHAME ambapo ni kiasi cha Milioni 200 ambazo wanaendesha mradi huo na wanaendelea na mrejesho kidogokidogo japo kumekuwa na changamoto mbalimbali.

Amemuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu katika mgao wa fedha kata ya Buguruni wameomba uangaliwe vizuri na halmashauri ya Jiji la dar es salaam kwasababu kata hiyo inakituo cha ukusanyaji wa mapato na wafanyabiashara waliowengi wa kata ya buguruni ndio wanaokusanya hayo mapato.

"Kwa mujibu wa taarifa yetu tumeonekana tumekusanya karibu milioni 200 na zaidi lakini mgawanyo tunaopewa hauzidi asilimia 10, kwahiyo tunaiomba halmashauri ya jiji la Dar es salaam na serikali Kuu waturejeshee mgao wenye kutosha". Amesema

Amesema miradi waliotembelea yote kwa asilimia kubwa ipo kwenye hali nzuri ila bado mradi mmoja ambao wataendelea kuujadili na kuweza kupata majibu ambao ni mradi wa TASAF ukiwa una Sintofahamu hasa kutokana na fedha zilizotengwa hazilingani na maendeleo yaliyopo kwenye mradi huo.

Nae Diwani Kata ya Buguruni Bw.Busoro Pazzi amesema katika kipindi kifupi, Kata ya Buguruni wamepatiwa zaidi ya shilingi Bilioni 5 katika miradi mbalimbali ya maendeleo na katika mradi wa mfereji ambao wametembelea umegharimu kiasi cha Bilioni 3.2

"Mradi huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kwasababu zamani kulikuwa na kero ya maji ya mvua kuingia katika makazi ya watu lakini kutokana na mradi huo kutekelezwa,suala mafuliko kwa kiasi kikubwa yamepungua katika mtaa huo". Amesema Bw.Pazzi.

Pamoja na hayo amempongeza Rais Samia kwa kuwapatia shilingi Milioni 360 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 18 vya madarasa katika shule ya sekondari Buguruni kwani awali walipatiwa shilingi milioni 220 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa kupitia mradi wa Uviko na sasa hivi kwenye pochi la mama wamepatiwa milioni 120 wamejenga vyumba sita vya madarasa.



Post a Comment

0 Comments