Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (kushoto) akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware (katikati) muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2025 kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.
**********************
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa mikakati iliyojiwekea kutekeleza malengo ya nguzo ya tatu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Mhe. Luvanda amesema hayo leo Alhamisi Machi 05, 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kujitambulisha na kuzungumza na Menejimenti ya Baraza hilo sambamba na kufahamu majukumu yanayotekelezwa na Ofisi hiyo.
Mhe. Luvanda amesema NEMC imebeba maono na matarajio makubwa ya nchi katika kufikiamalengo ya dira ya maendeleo ya taifa 2050 hususani utelekelezaji wa nguzo ya tatu inayoakisi masuala ya uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi.
“Kwa taarifa nilizoona nimeridhishwa na utayari wenu katika utekelezaji wa dira 2050…..Hatuna budi kutambua kuwa tumebeba matumaini ya Viongozi wakuu wa kitaifa katika kufanikisha utekelezaji wa Dira 2050 katika upande wa mazingira” amesema Mhe Balozi Luvanda.
Aidha Mhe. Balozi Luvanda amesema suala la elimu kwa umma halina budi kupewa kipaumbele na msukumo wa pekee ili kuhakikisha inapatiwa uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wakutunza na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya mustabali endelevu wa taifa.
Balozi Luvanda pia ameishauri Menejmenti ya NEMC kuweka msukumo wa kujitangaza kwa jamii na wadau mbalimbali kwa kuwa misingi ya utekelezaji wa jukumu hilo limeanishwa katika sheria na kanuni zinazosimamia majukumu ya taasisi hiyo.
Mhe. Balozi Luvanda amesema NEMC ni taasisi muhimu yenye mchango mkubwa katika kuharakisha kasi ya ukuaji wa sekta za maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini na hivyo ana imani na watendaji wa ofisi hiyo katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa maendeleo endelevu ya taifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware amemshukuru Mhe. Balozi Luvanda kwa ziara hiyo ya kikazi katika ofisi za baraza hilo na kuwa ofisi yake ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuwezesha na kufanikisha dhamira na maono ya Serikali.
“Sisi kama Watumishi wa NEMC tunakukaribisha Mhe. Balozi Luvanda tutambua majukumu uliyonayo yanaakisi shughuli zinazotelekezwa na NEMC, hivyo tupo tayari kupokea maelekezo na kufanyia kazi” amesema Dkt. Sware.
Mhe. Balozi Baraka Luvanda aliteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais akichukua nafasi ya Prof. Peter Msoffe aliyehamishiwa Wizara ya Kilimo.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akipokea shada la maua kutoka Bi. Florida Kavure Afisa Mazingira waBaraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akisalimiana na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa ziara yake ya kikazi kutembelea ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026 kuanza ziara yake ya kikazi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware.
Baadhi ya Watendaji Waandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhin a Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia kikao baina ya Ofisi hiyo na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda wakati wa ziara yake ya kikazi kutembelea Ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kemilembe Mutasa (kushoto) akifuatilia kikao baina ya Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Baadhi ya Watendaji Waandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhin a Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia kikao baina ya Ofisi hiyo na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda wakati wa ziara yake ya kikazi kutembelea Ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akifuatilia Makala mjongeo inayoelezea majukumu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhin a Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware akitoa taarifa ya utekelezaji wa Baraza hilo kwa Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Balozi Baraka Luvanda aliyefanya ziara ya kutembelea Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akizungumza na Viongozi na Watendaji waandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhin a Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiongozwa na Makurugenzi Mkuu, Dkt. Immaculate Sware (kulia) wakati wa ziara yake aliyoifanya katika ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam leo Jijini Machi 05, 2026.
Naibu Katibu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware wakati wa ziara yake aliyoifanya katika Ofisi za Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam leo Machi 05, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware (kulia) na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kemilembe Mutasa (kushoto) pamoja na watendaji wengine wa Baraza hilo muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya katika Ofisi zas Baraza hilo leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kutembelea ofisi za baraza hilo Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
(NA MPIGAPICHA WETU)














0 Comments