Ticker

6/recent/ticker-posts

LHRC YAIKUMBUSHA JAMII KUTOA USHIRIKIANO KUPINGA VITENDO VYA UKEKETAJI

Afisa Mwandamizi Dawati la Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu LHRC Wakili Getrude Dyabene akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2023 jijini Dar es salaam katika kuazimisha Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji.
Afisa Mwandamizi Dawati la Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu LHRC Wakili Getrude Dyabene akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2023 jijini Dar es salaam katika kuazimisha Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji. Afisa Mwandamizi Dawati la Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu LHRC Wakili Getrude Dyabene akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2023 jijini Dar es salaam katika kuazimisha Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji.



************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TANZANIA imeridhia mkataba wa kimataifa wa kupinga aina zote za ukatili kwa wanawake CEDDAW wa mwaka 1979 pamoja na mkataba wa nyongeza wa haki za wanawake wa Afrika maarufu kama Maputi Protocol uliosimamia kupingana na mila potofu ikiwemo ndoa za utotoni na ukeketaji.

Kuendelea kutumika kwa sheria hizi za kimataifa na kikanda kumezidi kutanua wigo wa sheria na uwajibikaji wa kitaasisi katika kulinda masilahi ya mtoto wa kike dhidi ya ukeketaji.

Ameyasema hayo leo Februari 23,2023, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) , Afisa Mwandamizi Dawati la Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu LHRC Wakili Getrude Dyabene wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za LHRC Jijini Dar es Salaam katika kuazimisha Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji.

Amesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali, Mashirika na Taasisi mbalimbali bado ukeketaji umeendelea kutekelezwa katika baadhi ya jamii.

"Kwa mujibu wa takwimu za taarifa ya Demographia na afya ya 2016 zinaonyesha kuwa pamoja na jitihada za kutokomeza vitendo hivyo, bado kuna mikoa mitano Tanzania inayoongoza kwa ukeketaji nchini ikiongozwa na Manyara wenye asilimia 58% ukifuatiwa na Dodoma wenye asilimia 47%, Arusha 41%, Mara 32% na Singida yenye asilimia 31%". Amesema

Aidha amesema mtandao wa mashirika yanayopinga ukeketaji hapa nchini umeendelea kusimama imara katika kuhakikisha kuwa ukeketaji unakoma ifikapo 2030 ili kuendana na mikakati ya maendeleo endelevu ya kidunia ya kuondoa aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto na vilevile kuendana na mikakati ya kitaifa kama ilivyoainishwa katika mpango kazi wa kitaifa wa kupinga vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema serikali imeendelea kuboresha sheria na sera mbalimbali ili kupanua wigo wa adhabu kwa wale wanaoendelea kutekeleza kitendo hicho cha kikatili.

Post a Comment

0 Comments