Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA BETIKA YAZINDUA KAMPENI YA "MTOKO WA KIBINGWA"

Meneja wa Kampuni ya Mchezo wa kubashiri Betika Tumaini Maligana (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2023 Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Kampuni ya Mchezo wa kubashiri Betika Tumaini Maligana akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7,2023 Jijini Dar es Salaam.

*********************

KAMPUNI ya Mchezo wa kubashiri Betika wazindua rasmi Kampeni yake ya "Mtoko wa Kibingwa" kwa Msimu wa 5 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 07,2023 Jijini Dar es salaam Meneja wa Kampuni ya Betika Tumaini Maligana amesema Kampeni hiyo imeanza rasmi leo 07,2023 na kutarajiwa kuhitimishwa rasmi April 16,2023 siku ya Derby ya Simba na yanga.

Hata hivyo amesema Kampeni hiyo ni Msimu wa 5 ambapo itaendesha droo yake kila wiki na kuchukua washindi 10 hadi kukamilika kwa washindi 100.

Pia ameeleza utofauti wa Msimu wa 5 ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya washindi kuliko misimu iliyopita pamoja na kuwapa fursa washindi kushuhudia Mechi kubwa ya derby ya 3 Afrika .

Post a Comment

0 Comments