Ticker

6/recent/ticker-posts

MIFUGO YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 1.5 YAGAIWA KWA WANANCHI JIMBONI MUFINDI


MIFUGO yenye thamani ya Sh bilioni 1.5 imegawaiwa kwa wananchi wa Kata ya Nyololo na Maduma katika Jimbo la Mufindi Kusini ikiwa ni utekekezaji wa agenda ya 'One family one catle'.

Mifugo hiyo iliyotolewa na Shirika la World Vision ni Ng’ombe 600, Nguruwe 600 na Kuku 4,000

Akizungumza leo Februari 14,2023, Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile amesema ugawaji wa wanyama hai kwa wananchi lengo ni kupambana na utapiamlo na kuimarisha lishe kwa wananchi.

"Mifugo hii pia itasaidia kuongeza kipato kwa wananchi, kuhamasisha ulimaji wa nyasi za malisho hivyo kuzuia kilimo kwenye vyanzo vya maji, Samadi itatumika Shambani hususani kwenye Parachichi, Mahindi na mazao mengine."Amesema na kuongeza

"Pia ni maandalizi ya uzalishaji nishati ya Biogas, kutoa uhakika wa malighafi viwandani ikiwemo maziwa, ngozi, nyama pamoja na kwato."

Aidha, Kihenzile amewataka wananchi wa Mufindi Kusini kuunganisha nguvu katika kuboresha afya na uchumi.

Kihenzile pia amelishukuru Shirika la World Vision kwa kutoa wanyama wenye thamani ya Tshs 1.5bilion na pia kuwashukuru wadau wengine ambao wako kwenye Mkakati wa utekelezaji wa kuunga Mkono jitihada hizo ikiwa ni pamoja na Shirika la Land O’Lakes, Benki ya Kilimo, Water For Africa, Halmashauri ya Mufindi, aidha ameomba wadau wengine kuunga mkono Agenda hiyo ili kuweza kuwafikia wananchi mbalimbali kwenye Kata zote 16

Post a Comment

0 Comments