Ticker

6/recent/ticker-posts

OPERESHENI KABAMBE UKAGUZI VYOMBO VYA MOTO KUANZIA FEBRUARI 6 -MACHI 13.



Mkuu wa Kikosi cha Usalam Barabarani Ramadhani Ng’anzi akipeana mkono na mwakilishi wa Udhimini wa opereshi hiyo Kabambe Mkuu wa Kitengo cha Bima kutoka Benki ya NMB Martini Masawe katika makao Makuu ya Polisi Trafiki Jijini Dar es saalam

****************

Na Magrethy Katengu

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litahakikisha linadhibiti ajali za barabarani zinazotokea hususa ni wakati wa usiku na kusababisha vifo vya watu na majeruhi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkuu wa Kikosi cha Usalam Barabarani Ramadhani Ng’anzi amesema kampeni ya Uzinduzi operesheni ukaguzi wa vyombo vya moto watakagua ikiwemo magari bajaji pikipiki na zoezi hilo litahitimishwa Machi 13 mwaka huu.

"Katika tathimini yetu tumegundua kuwa ajali nyingi hutokea wakati wa usiku asilimia kubwa ni magari ya kubeba mizigo kugongana na magari ya abiria binafsi hivyo operesheni yetu kabambe itafanyika muda wote"amesema SACP Ng'anzi.

Ng'azi amesema lengo la ukaguzi huo ni kuhakikisha kunakuwepo usalama wa vyombo vya moto ili kupunguza ajali za Barabarani hivyo na kusaidia vyombo vyote vya Barabarani vinakuwa salama tutahakukisha ukaguzi unafanyika kuanzia kwenye breki,Mifumo ya umeme.

Pia Ng'anzi amesema lengo la kufanya ukaguzi wa magari hayo ametumia fursa hiyo kuwaagiza Wakuu wa Vikozi vya Usalama Barabarani (RTO) Mikoa kutenga maeneo ya ukaguzi huo kuanzia leo na kuwataka madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuonyesha ushirikiano Februari 6 hadi machi 13 wiki ya Maadhimisho ya Usalama Barabarani 

"Wiki ya usalama barabarani inatanguliwa na ukaguzi wa magari na utoaji wa elimu kwa watumiaji wa barabara kwahiyo matarajio yangu madereva wote kuanzia yanayobeba abiria,mizigo ,magari ya mafuta ,magari yanayobeba wanafunzi yaliyokaguliwa hivi karibuni,pikipiki,bajaji wanaweza kufika katika kituo cha Polisi kwaajili ya ukaguzi na Jeshi la Polisi litatoa hati maalumu kuonyesha kwamba chombo hiko kimekaguliwa na inavigezo vya kuingia barabarani "amesema SACP Ng'anzi.

Sanjari na hayo Kikosi cha usalama kitaendesha ukaguzi huo na itahitajika gharama za mchango ambapo kwa magari ya biashara shilingi 7000, magari binafsi shilingi 5000, Bajaji na Pikipiki shilingi 2000 hivyo ukaguzi huo ni kuhakakikisha usalama wa wananachi na mali zao unakuwepo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Bima kutoka Benki ya NMB Martini Masawe amesema Benki hiyo imetoa udhamini katika Operesheni Kabambe kwa kuwa wanaguswa na ajali zinazotokea hivyo wataendelea kuunga mkono suala hilo ili kusaidia ajali zinapungua kabisa.

Aidha Kikosi cha Usalama Barabarani kimetoa pole kwa wanafamilia wote waliopoteza ndugu zao usiku wa kuamkia Jumamosi Tanga wakati wakitokea Dar es salaam kuelekea Moshi kwa mazishi hivyo wanawaombea majeruhi wote wapone warudi katika hali yao.
Mkuu wa Kikosi cha Usalam Barabarani Ramadhani Ng’anzi akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 6,2023 mJijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kikosi cha Usalam Barabarani Ramadhani Ng’anzi akizindua operesheni kabambe ya ukaguzi wa vyombo vya moto Jijini Dar es salaam

Post a Comment

0 Comments