Ticker

6/recent/ticker-posts

ULEGA ARIDHISHWA NA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA KATIKA JIJI LA TANGA CHINI YA USIMAMIZI WA TANGA YETU


Na Oscar Assenga,TANGA



Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Leo amefanya ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya JijiTanga na Kufurahishwa na Kasi ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri Chini ya Usimamizi wa Tanga Yetu.

Miradi hiyo ya Maendeleo ambayo Ulega amefurahishwa nayo ni pamoja na Mradi wa Kilimo Cha Mwani na Ufugaji wa Tango Bahari ( Jongoo Bahari) ulio chini ya kikundi Cha Mchukuuni Tanga Jiji chenye Wanachama 36, Mradi wa urutubishaji Samaki aina ya kaa na Vizimba vya kufugia Samaki hao zaidi ya 600 kwa Wakati mmoja pamoja na Mradi wa Utotoreshaji wa Vifaranga 10,000 kwa Wakati mmoja Wenye Vijana 50 .

Miradi hiyo inaratibiwa na kusimamiwa na Tanga Yetu kwa ufadhili wa Fondation Botnar kwaajili na kuipeleka Tanga kwenye Uchumi wa Bluu kupitia mafunzo ya vitendo yanayoleta Ajira kwa Vijana na Wanawake.

Ulega aliwapongeza Wasimamizi wa Miradi hiyo kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kuwatumikia Wananchi,

" Niwapongeze Sana wote mnaowatumikia Wananchi wetu kwa moyo wa kujitoa hususani nyie Wadau Wa Maendeleo Tanga Yetu na Fondation Botnar, Niwaagize Maofisa Uvuvi na Mifugo muhakikishe Mnawatembelea Wanavikundi Hawa na kuwasaidia kero zao, Nimesikia kero ya Baadhi ya Wavuvi kuwa Wanafanya Uharibifu kwenye mashamba ya Mwani , naomba muwakamate na muwafikishe kwenye vyombo vya Sheria na mfanye Doria za Mara kwa Mara ili muwabaini Wahalifu wanaorudisha nyuma Maendeleo ya Wananchi wa Hali ya chini" Alisema Ulega

Ulega Alisema serikali imeweka Shilingi Bilioni 2.5 kwa ajili ya kuendeleza zao la mwani ambapo tayari Sh. Milioni 447 zimeshatolewa kwa vikundi mbalimbali na Sh. 11.5 Bil. zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza boti za kisasa za uvuvi na Shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba vya kufugia samaki aina ya sato kwenye Ziwa Victoria.

Ulega alisema Serikali imejizatiti kuinua uchumi wa buluu kwa kutenga fedha nyingi huku wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakikaribishwa kuunga mkono jitihada hizo kwaajili ya kuweka mazingira mazuri ya ukuzaji viumbe maji na kuongeza Ajira kwa katika Jamii hususani kwa Vijana.

Aidha, aliwataka wadau wa Sekta ya Uvuvi hususan vikundi vya ushirika vya wavuvi kuchangamkia fursa ambayo serikali imetoa fedha ili kuongeza mahitaji ya ukuzaji viumbe maji kutokana na masoko yaliyopo ndani na nje ya nchi.

Maagizo hayo ya kukamatwa kwa Baadhi ya Wavuvi wanaofanya uharibifu kwenye mashamba ya Mwani na maeneo ya Ufugaji wa Matango Bahari yanafuatia Baada ya Mwenyekiti wa chama Cha Ushirika wa kilimo cha mwani na ufugaji Matango Bahari cha Mchukuuni Jijini Tanga, Abdallah Mtondo Kulalamikia kitendo cha baadhi ya watu ambao siyo waaminifu kuiba matango bahari katika mashamba yao hususan nyakati ambapo maji yamefunika mashamba hayo.

Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu hao ambao wamekuwa wakiwarudisha nyuma katika shughuli za ufugaji ili kujiongezea tija jambo ambalo Naibu Waziri Ulega amelitolea kauli kali na kutaka mamlaka husika kuingilia kati jambo hilo huku akisisitiza wanunuzi wa mwani na tango bahari kununua mazao hayo kwenye vikundi vinavyotambulika na kusajiliwa.

Post a Comment

0 Comments