Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA SC YAONDOKA NA MAMILIONI YA MAMA, YAICHAPA 3-1 TP MAZEMBENA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya timu ya TP MAzembe ya nchini DR Congo baada ya kuichapa kwa mabao 3-1 kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Yanga katika mchezo huo waliweza kutawala katika kipindi cha kwanza ambapo walifanikiwa kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa nyota wao Kennedy Musonda dakika 7 na Mudathir Yahaya kufunga dakika ya 11.

Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wanajiamini hivyo kuwafanya TP Mazembe wachezee mpira na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Alex Ngonga aliepiga mpira wa adhabu na kutinga nyavuni.

Bao la tatu limefungwa na Tusila Kisinda dakika ya 91 ya mchezo baada ya kuingia akitokea benchi

Post a Comment

0 Comments