Ticker

6/recent/ticker-posts

COSTECH YAMUIBUA MTAFITI NA MBUNIFU WA KUTENGENEZA CARBONE KUPITIA VIFUU VYA NAZI


MIONGONI vya visababishi vya vizalia vya mbu kwenye makazi yetu ya kila siku ni uchafu ambao unatokana na vifuu vya nazi, watumiaji wa nazi wakishatumia nazi lile gamba lake (kifuu) ukitupa na kuweza kufanya mbu kuzaliana.


Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali ambazo zinaibua bunifu ambazo zinakuwa msaada mkubwa kwa jamii zetu hasa kiuchumi.
COSTECH imemuibua Mtafiti na mbunifu wa Teknolojia ya kutengen eza Carbone kupitia vifuu vya nazi ambavyo hukusanya mtaani na kuvikusanya pamoja.


Mtafiti na Mbunifu wa teknolojia hiyo Bw.Tiberius Mario akizungumza mbele ya waandishi wa habari waliotembelea eneo lake la kutengenezea carbone, amesema vifuu vya nazi vinakazi kubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza carbone inayotumika kuchenjulia madini na kusafisha maji.


Amesema ubunifu huo alioufanya unanafasi kubwa ya kudhibiti uchafunzi wa mazingira kupitia vifuu vya nazi na pia kuepusha magonjwa kama malaria na kipindupindu.


”Tunatengeneza Activated Cardbon kutoka katika vifuu vya nazi,Carbon ni vichembe vidogovidogo tunatengezea matundu ndani vinakuwa na corosty ndani hivyo vitundu vinatumika kukamatilisha dhahabu.


“Nimeegemea sana kwenye upande wa dhahabu na maji machafu ninabadilisha kifuu cha nazi kwenda kwenye Carbon ambayo kwenye migodi yote Tanzania hauwezi kupata dhahabu bila ya kuwa na Carbon ni Udongo baada ya kuchujwa lazima ipitishwe kwenye carbon dhahabu zitoke kwenye udongo,”amesisitiza.


Amesema hapa nchini hakuna kiwanda cha kutengeneza Carbon kwa asilimia 100 zinatoka nje ya nchi huku mikoa ya Pwani na Kusini kuna nazi nyingi zaidi ya tani 350000 kwa mwaka ambapo hutoa vifuu vingi.


Mario amesema Kidunia wanaoongoza kwa zao la nazi ni Indonesia,India na Tanzania iko namba 16 ambao inazalisha nazi tani 382,164 kwa mwaka kiasi ambacho kinaweza kuzalisha vifuu vingi.


“Kama vifuu vilisipoangaliwa vizuri vinaweza kusababisha magonjwa mfano ukiacha vikanyeshewa na mvua mbu wake watakapokuu malaria yake ni kali pia uchafu unaokuwa katika kifuu cha nazi akitoa kipindupindu inaweza kutokea hivyo kubadilisha kunapunguza uchafuzi wa mazingira.


Amesema katika nchi kwa inaagiza nje Carbone zaidi ya tani 1500 kwahiyo inapoteza kiasi kingi ambazo ni dola milioni 6.7 .


“Mimi natumia kiwango kidogo ya vifuu 0.1 ya mimi ninachotumia nchini tunanunua nje wenzetu wanajua kutumia vifuu hiyo ninayotengeneza inaenda kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madili kwani zinagharama nafuu na kuna wakati migodini zinaadimika mfano wakati wa corona,”ameeleza Mario.


Aidha amefafanua kuwa Carbone hiyo imeweza kupimwa katika maabara na utendaji wake ni asilimi 98 katika madini na maji asilimia 98 .


Pia amesema chanzo cha joto anayotumia ni makaa ya mawe na kuni ambapo kitaalamu anahitaji joto zaidi ya 300,000 lakini kuni inanipa joto la 4000 kwa kilo moja ili kupata 300000 ninatumia kuni nyingi na muda ni mrefu.

Post a Comment

0 Comments