Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA MRADI WA KITEGAUCHUMI CHA JENGO LA KIBIASHARA (THE ROCK CITY MALL) LA PSSSF

NA MWINDISHI WETU, MWANZA

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee PIC) imepongeza uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Mradi wa kitegauchumi cha jengo la kibiashara (the rock city mall) jijini mwanza.

Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa PIC, Mhe. Jerry Silaa wametoa pongezi hizo Machi 30, 2023 baada kutembelea mradi huo kwa lengo la kuona tija iliyopo kwenye uwekezaji huo.

Walisema uwekezaji wa jengo hilo umebadilisha sura ya jiji la Mwanza ambapo zamani eneo hilo lilitapakaa vibanda tu na kwamba uwekezaji umebadilisha sura ya jiji la Mwanza jambo ambalo limeleta thamani ya kijamii (social value),” alisema

Aidha wamesema uwekezaji wa mradi wa “the rock city mall” ni moja ya miradi iliyokamilika na yenye kutia matumaini hata hivyo walishauri kufanywe marekebisho sehemu ambazo zina mapungufu ili kuvutia wapangaji kwenye maeneo ambayo bado hayana wapangaji.

Walioungana na Menejimenti juu ya athari za ugonjwa wa Korona (COVID-19) kwenye Biashara ambapo umeleta mtikisiko wa uchumi Duniani biashara nyingi zimeanguka au kusua sua na hivyo wakashauri nafasi ambazo bado hazijapata wapangaji kutokana na bei ya pango menejimenti ikae na kuangalia upya viwango hivyo vya kodi ya pango.

Aidha licha ya kupongeza uwekezaji huo pia walisema ripoti ya mradi imekaa vizuri na hasa kwa Kamati inayoangalia Uwekezaji wa Mitaji ya Umma na Vipindi vya Miradi kuanza Kuingiza Faida iliyokusudiwa.(Payback period).

Mwenyekiti wa PIC Mhe. Jerry Silaa licha ya kupongeza amebainisha kuwa pesa zilizowekezwa kwenye miradi ni pesa za wanachama na sio za serikali hivyo akashauri umakini ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

“mbele ya safari wajumbe tutakaa na kufanya uchambuzi kuona uwekezaji wa jumla wa sasa wa Mfuko ili kuwa na hakika ya uwekezaji wenye tija.” Alifafanua.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF Dkt. Aggrey Mlimuka alisema Bodi yake imepokea ushauri wa Wajumbe na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo hayo ili kuongeza tija katika uwekezaji huo.

“Bodi imeweka mikakati ya kuweza kufanya maamuzi ya kibiashara ambayo yanapaswa kufanyika mara kwa mara kulingana na wakati uliopo” Alisema Dkt. Mlimuka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema Jengo lina eneo la upangishaji lenye sqm 21,151.82 ambapo hadi mwezi Febrauri 2023 kampuni imeweza kupangisha jengo kwa kiwango cha asilimia 82%.

Alisema maeneo ambayo tayari yamepangishwa kwa ujumla yana meta za mraba 17,436.07; kwa upande wa maeneo ambayo bado hayajapangishwa yana ujumla ya meta za mraba 3,715.75 ambayo ni sawa na asilimia 18%.

Hata hivyo tayari wapo waombaji ambao wamechukua offer kwa baadhi ya maeneo hayo ikiwemo, vyumba kwa ajili ya maduka, na ofisi mbali mbali na tayari tulishatoa maelekezo ya jinsi ya kujaza nafasi zilizobaki wazi ikiwa ni pamoja na kupata wapangaji wakubwa na tayari wameanza kupatikana na kutolea mfano Woolworth.

Aidha kuhusu wapangaji ambao wana madeni ya pango alisema kumekuwepo na maendeleo mazuri ya ulipaji kwa wale wanaodaiwa baada ya ugonjwa wa Korona (Covid19).

“Wateja wapya wanaoingia sasa tumekubaliana wanalipa kila baada ya miezi mitatu (3), miezi 6 na mwaka mzima, hilo limetusaidia kwa kiasi kikubwa.” Alifafanua CPA. Kashimba.

Jengo la The Rock City Mall linamilikiwa na Kampuni inayojulikana kama Mwanza City Commercial Complex Company Limited (MCCCCL). Kampuni hii imeundwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF), Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halimashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Awali ubia ulikua kati ya LAPF na Jiji la Mwanza na baada ya mgawanyo wa Jiji la Mwanza na kuundwa kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Hivyo basi mradi huu sasa unamilikiwa na wabia watatu ambao ni Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Alisema CPA. Kashimba wakati akiwasilisha ripoti ya uwekezaji .

Alisema PSSSF ina miliki asilimia 90 na wabia wengine wanamiliki asilimia 10 ya hisa, kwa mchanganua wa Halmashauri ya jiji la Mwanza (MCC) kumiliki asilimia 6 na Manispaa ya Ilemela (IMC) wanamiliki asilimia 4 ya hisa hukuthamani ya mradi kwa maana ya uwekezaji ni shilingi bilioni 80.

Mwenyekiti wa PIC Mhe. Jerry Silaa
Mhe. Silaa (katikati) akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi yaWadhamini ya PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba na wajumbe wengine wa Kamati wakitembelea mradi wa jengo la kibiashara la the Rock City Mall jijini Mwanza Machi 30, 2023.
Mkurugenzi Mkuu PSSSF, CPA. Hosea Kashimba
Mhe. Silaa (katikati) akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi yaWadhamini ya PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba na wajumbe wengine wa Kamati wakitembelea mradi wa jengo la kibiashara la the Rock City Mall jijini Mwanza Machi 30, 2023.


Post a Comment

0 Comments