Ticker

6/recent/ticker-posts

EWURA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WILAYANI KONDOA


Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mkoani Dodoma maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”yamefanyika katika Wilaya ya Kondoa.


Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani ambapo mkoani Dodoma maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”yamefanyika katika Wilaya ya Kondoa.

Na.Alex Sonna-KONDOA

Wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuungana na wanawake wengine kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi katika maadhimisho ngazi ya Mkoa, yaliyofanyika wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Maadhimisho hayo yamefunguliwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule, na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bw. Hamis Mkanachi na Mbunge wa Kondoa Bi. Ashatu Kijaji pamoja na viongozi wengine kutoka mkoa wa Dodoma wameshiriki maadhimisho hayo.

Maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia katika Kuleta Usawa wa Kijinsia”, huku kauli mbiu ya EWURA ikiwa, “Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji: Chachu katika Kukuza Uchumi na Maendeleo kwa Taifa”

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule amewataka wanawake kujikita katika kutafuta taarifa za fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali.'

Amesema kuwa bado zinahitajika jitihada za kumsaidia mwanamke kwani viongozi wanawake bado ni wachache.

'Niwaomba wanawake wote mlioshiriki katika maadhimisho haya mjiunge katika vikundi ili iwe rahisi kukopesheka''amesema RC Senyamule

Hata hivyo Bi.Senyamule amezipongeza Taasisi za Serikali na Binafsi zilizoshiriki maadhimisho hayo ngazi ya Mkoa.

Post a Comment

0 Comments