Ticker

6/recent/ticker-posts

MKOA KAGERA WANG'ARA NDANI YA MIAKA MIWILI YA DKT SAMIA.
*************************


Na Shemsa Mussa .Kagera


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Albert John Chalamila ameitumia siku moja muhimu kuyasema yale mema aliyoyafanya Mhe Rais Samia.ndani ya miaka miwili ya utawala wake.


Rc Chalamila ametumia siku hiyo ya hafla kumpongeza Rais na kuwakumbusha wananchi yale mema aliyoyafanya Dkt samia ndani ya kipindi cha miaka miwili ya utawala wake ambapo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mayunga Manispaa ya Bukoba .


Amesema katika kuimalisha sekta ya elimu mkoani kagera serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imetoa shiling Bilion 17 na Milion 500 za awali kwa ajili ya ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kitakachojengwa katika kata ya karabagaine halmashauri ya Bukoba kwa ekari 314.


" Lakini licha ya kuwa na maendeleo yote haya tunakuomba sana Mhe Rais utusaidie kufungua vyuo vilivyofungwa kwa muda mrefu ili sekta ya elimi ipanuke na kukua zaidi, amesema Chalamila."


Aidha mkuu huyo amesema serikali imejenga vyumba vya madarasa 1,395 kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza vilijenjwa vyumba 881 na kumalizia vyumba 514 pamoja na ujenzi wa shule mpya 8 kila wilaya shule moja kwa ghalama ya Bilion 8 .


Katika sekta ya afya zilitengwa Bilion 40 kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za afya ikiwemo kujenga hospitali za wilaya katika kila halmashauli zote ndani ya mkoa.Sanjari na hayo ameeleza kuwa pia ameleta mashine katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo CT-SCAN yenye thamani ya bilioni 1.8 na kuwaondolea wananchi adha ya kwenda Bugando mkoani mwanza kwa kipimo hicho.


Rc Chalamila ameongeza kuwa mkoa wa kagera umekuwa ukipokea kiasi cha shiling Bilion 1 na Milion 600 kila mwezi kwa ajili ya utoaji elimu bure huku ikilipa ada pamoja na posho kwa watumishi huku shule 12 zilizochakaa zikikarabatiwa kwa Bilion 8 na hivyo kuwaomba wananchi hasa wanawake kuendelea kumuamini Rais kwa kile anachokifanya .


" Mimi ni Mwanaume nitawashangaa sana wanawake mkimnyang'anya kijiti mwanamke mwenzenu mnatakiwa mwendelee kung'ang'ania kushikilia nafasi hiyo mpaka mchoke wenyewe.amesema chalamila ."
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera (RAS ),Toba Nguvila,ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita inasimamia utekelezaji wa ilani ya mwisho katika utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa malengo ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),katika kustawisha maisha ya watanzania na kutokomeza umasikini.

Nguvila, ameeleza kuwa serikali chini ya usimamizi wa Rais Samia, imeweza kutekeleza vyema ilani ya CCM ya mwaka 2020 kwa kutekeleza maeneo sita ya vipaumbele kama kulinda na kuimarisha misingi ya utu,usawa ,haki na uongozi bora na kudumisha amani umoja na mshikamano wa taifa.

Baadhi ya wananchi waliofika katika hafla hiyo wamesema wanamshukuru Rais Samia kwa kuuona na kuupa kipaumbele kikubwa mkoa wa kagera na kuupatia fursa zinazopatikana katika sekta mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments