Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF. MBARAWA- LIPENI KODI KWA WAKATI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo
kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakati alipozindua nyumba za
makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian Village
Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Bw. Ludovick Nduhiye akizungumza na Wananchi
wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa nyumba
za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian
Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakimsikiliza
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani)
wakati alipozindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo
Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akifurahia jambo na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro
mara ya kuzindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo
Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es
Salaam.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro
kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo
Magomeni Kota na Kanadiani Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es
Salaam, kabla ya Waziri huyo kuzindua nyumba hizo.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi
mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Ujenzi akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa wa nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na
Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam, kabla ya
Waziri huyo kuzindua nyumba hizo.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa malekezo
kwa Viongozi wa Wizara na Taasisi kabla ya kuzindua ujenzi wa nyumba za makazi
za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian Village Msasani
Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam, kabla ya Waziri huyo kuzindua nyumba hizo.


Muonekano wa jengo la nyumba za Watumishi wa Umma ambalo limejengwa katika
eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Saalaam.

…………………………………..

Serikali itaendelea kuuwezesha Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kujenga
nyumba za kisasa kwa ajili ya watumishi wa Umma na za kibishara ili
kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya nyumba yanayoongezeka siku kwa siku
nchini.

Akifungua Majengo kwa ajili ya makazi kwa watumishi wa Umma katika eneo
la Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula Masaki jijini Dar es
Salaam Waziri wa Ujenzi na Uchkuzi Profesa Makame Mbarawa amesema nia
ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake wanaishi katika makazi yaliyo bora
na hivyo kuleta tija na ufanisi katika kazi za Umma.

“Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha watumishi wanapata makazi salama na ya
kisasa yanayoendana na sayansi na teknolojia., hivyo TBA hakikisheni
wapangaji wote watakaopata nafasi ya kuishi kwenye nyumba hizi wanalipa
kodi kwa wakati’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema Serikali inatambua umuhimu wa makazi bora kwa
wananchi wake ambapo mahitaji ya nyumba bora yanakadiriwa kuwa zaidi ya
nyumba milioni tatu kwa nchi nzima hivyo Serikali itaendeelea kujenga nyumba
za ghorofa zitakazoweza kuhudumia watumishi wengi katika eneo dogo.

Waziri Prof Mbarawa amewtaka TBA kuhakikisha watakaopanga kwenye
nyumba hizo wanazitunza kwa kuzingatia kanuni za usafi na matumizi bora ya
nyumba ili zidumu kwa muda mrefu.

“Watakaoshindwa kulipa kodi kwa wakati watoeni muweke wengine tunataka
nyumba hizi ziweze kukusanya fedha na fedha hizo hizo zitumike kujenga
nyumba nyingine nyingi zaidi’ amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi, Bw. Ludovick Nduhiye amesema Wizara
itaiwezsha TBA kwa kuipa fedha ili kutimiza malengo ya Serikali .

Kwa upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miudombinu, Mhe Selemani Kakoso ameipongeza Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi kwa namna inavyofanya kazi kwa ubora na ubunifu na kuitaka
Wizara kuiwezesha TBA kukusanya madeni wanayodai watumishi mbalimbali
ili kujiimarisha kiuchumi na kujenga miradi mingine.

“Mfumo mpya mliuoanzisha sasa wa kukusanya kodi ambao utamuwezesha
mwenye nyumba kulipa kodi kwa wakati utasaidia kupata makusanyo kwa wakati na hivyo kutimiza malengo hivyo uendelezeni’ amesisitiza Mhe.
Kakoso. 

Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema ujenzi wa nyumba za
kisasa katika maeneo ya Magomeni kota na Canadian village jijijini Dar es
Salaam ni mwendelezo wa Wakala huo kujenga nyumba za watumishi katika
maeneo mbalimbali nchini ambapo miradi kama hiyo inaendelea katika eneo la
Nzuguni-Dodoma, Mtwara, Shinyanga, Kilimanjaro na Kagera lengo likiwa
kukabiliana na upungufu wa nyumba bora kwa watumishi wa umma.

Zaidi ya Shilingi bilioni kumi zimetumika katika ujenzi wa miradi miwili ya
Magomeni Kota na Canadian Village na nyumba hizo zina uwezo wa
kuhudumia familia 28 kwa wakati mmoja.

Post a Comment

0 Comments