Ticker

6/recent/ticker-posts

TIMU YA VIJANA YA SIMBA SC YALAMBA DILI LA SH.MILIONI 500 KUTOKA MobiAd AFRIKA

Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba Bw.Salim Mhene, Mkurugenzi wa klabu ya Simba Bw.Imani Kajura , Mkurugenzi wa MobiAd Africa, Bw. Rumisho Shikonyi na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa MobiAd Africa, Bw.Norbet Leon wakionesha mfano wa hundi ya shilingi Milioni 500 zilizokabidhiwa kwa klabu ya Simba kutoka kwa Kampuni ya MobiAd Africa ambayo itaidhamini timu ya vijana ya Simba kwa miaka miwili. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 23,2023 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Klabu ya Simba Bw. Imani Kajura (kushoto) na Mkurugenzi wa MobiAd Africa, Bw. Rumisho Shikonyi wakisaini mkataba wa makubaliano wa miaka miwili kudhamini timu ya vijana ya Simba Sc. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 23,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba Bw.Salim Mhene akiwa pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa MobiAd Africa, Bw.Norbet Leon wakiwa wameshika jezi ya timu hiyo ikiwa na nembo ya mdhamini mkuu mpya MobiAd Africa ambao wameingia mkataba wa miaka miwili wa udhamini timu ya vijana wa timu hiyo. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 23,2023 Jijini Dar es Salaam


Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa MobiAd Africa, Bw.Norbet Leon akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa miaka miwili Kampuni ya MobiAd Africa kudhamini timu ya vijana ya Simba. mkataba huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 500 za Kitanzania.

Mkurugenzi wa MobiAd Africa, Bw. Rumisho Shikony akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa miaka miwili Kampuni ya MobiAd Africa kudhamini timu ya vijana ya Simba. mkataba huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 500 za Kitanzania.

Mkurugenzi wa Klabu ya Simba Bw. Imani Kajura akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa miaka miwili Kampuni ya MobiAd Africa kudhamini timu ya vijana ya Simba. mkataba huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 500 za Kitanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba Bw.Salim Mhene akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa miaka miwili Kampuni ya MobiAd Africa kudhamini timu ya vijana ya Simba. mkataba huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 500 za Kitanzania.


**************************

Na Magrethy Katengu

Klabu ya Simba Sport imeingia mkataba wa makubaliano na Kampuni ya MobiAd Africa kudhamini timu ya vijana ya Simba Sc wenye thamani ya shilingi milioni 500 ikiwa ni miongoni mwa malengo yao katika kuboresha timu ya vijana.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo imefanyika leo Machi 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa klabu ya Simba Bw.Imani Kajura amesema Soka la vijana ni muhimu sana. Ili uwe na timu ya vijana iliyo bora lazima iwezeshwe kama ilivyo kwa wachezaji wengine waliopita kwenye timu hiyo ya vijana.

Amesema Simba inakwenda mbele kutambua vipaji, kuvichukua na kuviendeleza na kuweza kutengeneza timu yenye vipaji vikubwa, na wanaamini Simba imara yenye vipaji haitaisaidia Simba pekee bali hata taifa letu.

“Leo tupo kwenye historia nyingine ya kuendeleza soka la vijana Tanzania. Mfumo wetu utakuwa mfumo wa wazi na endelevu.”- CEO Imani Kajula.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba Bw.Salim Mhene amesema program hii inayoitwa the future is now inalenga kuwakusanya vijana wengi zaidi wenye vipaji vya mpira wa miguu kwa kuwafundisha sambamba na kutengeneza taifa lenye soka linalotambulika ndani na nje ya nchi kupitia klabu hiyo ya Simba.

"Jambo hili ni kubwa lina neema na baraka natoa Shukrani za dhati MobiAd Afrika kwa kukubali kuidhamini timu yetu hii ya vijana hivyo tunawaahidi fedha hizi walizozitoa tutazitumia kwa mlengo uliokusudiwa "amesema Mhene.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa MobiAd Africa, Bw.Norbet Leon ameipongeza Simba kwa kuwa na mpango huo mkubwa ambao utawasaidia huko mbeleni na kuwaibua mastaa wengine ambao wataenda kusaidia klabu hiyo na timu ya taifa.

Post a Comment

0 Comments