Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na wawakilishi wa Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania uliongozwa na Kiongozi wa Programu Endelevu ya Mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Bw. Euan Davidson. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
*****************
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha vipaumbele vya Ajenda ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi vinapewa msukumo katika majukwaa ya Kitaifa na Kimataifa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Muyungi wakati wa mazungumzo baina yake naKiongozi wa Programu Endelevu ya Mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Euan Davidson.
Dkt. Muyungi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan imeweka mikakati na mipango mahsusi ya kitaifa kuhusu masuala ya mazingira na tabianchi ambayo inahitaji msukumo na ushirikiano wa karibu na wadau wa maendeleo.
Ameitaja mikakati hiyo ni pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambapo nguzo ya tatu inaelezea kuhusu masuala ya uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, juhudi zinazolenga kuiwezesha Tanzania kufikia nchi ya kipato cha kati ngazi ya juu ifikapo 2050.
Aidha Dkt. Muyungi amesema kipaumbele kingine kilichopewa msukumo ni pamoja na biashara ya kaboni, ambapo Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wadau na kwakuandaa utaratibu wa kitaifa na kimataifa kwa kuanzisha Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni (NCMC).
“Tanzania tayari ina kanuni na miongozo ya biashara ya kaboni na Kituo cha NCMCtayari kimeanza kazi kikiwa na bodi ya wakurugenzi na kamati ya wataalamu ya uchambuzi wa miradi ya kaboni” asema Dkt. Muyungi.
Dkt. Muyungi ametaja kipaumbele kingine cha Serikali kupitia hifadhi ya mazingira ni pamoja na mkakati wa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo kinara wa kampeni hiyo kitaifa na kimataifa ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akifafanua zaidi, Dkt. Muyungi ameeleza kuwa Tanzania pia inaendelea na utekelezajina Mchango wa tatu wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NDC 3) ambao umeandaliwa kwa ajili ya kupunguza uzalishaji wa gesi joto na kujenga ustahimilivu wa mazingira.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Programu Endelevu ya Mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Bw. Euan Davidson amesema Ubalozi huo upo tayari kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais ili kufanikisha ajenda ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Kiongozi wa Programu Endelevu ya Mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Euan Davidson (kushoto) akizungumza jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.



Mshauri wa masuala ya mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza Bw. Abdallah Shaha(kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Ubalozi huo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza jambo wakati kikao chake na wawakilishi wa Ubalozi wa Uingereza uliongozwa Kiongozi wa Programu Endelevu ya Mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Bw. Euan Davidson. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 05, 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa wa Programu Endelevu ya Mazingira kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Euan Davidson muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazunngumzo baina yao yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam leo Alhamizi Machi 05, 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Ubaloziw a Uingereza nchini Tanzania muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazunngumzo baina yao yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam leo Alhamizi Machi 05, 2026.
(NA MPIGAPICHA WETU)







0 Comments