Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA KAMATI YA AMANI WAPONGEZA OFISI YA MKUU WA MKOA MWA MWANZA KUANZA KUCHUKUA HATUA YA KUTOA ELIMU KUHUSU UGONJWA WA MARBURG




Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza Dkt.Jacob Mutashi na Askofu Robert Bundala wameipongeza Serikali ya Mkoa huo kwa kuanza kuchukua tahadhari za makusudi katika kutoa elimu ya kupambana na virusi vya ugonjwa hatari wa Marburg endapo utajitokeza.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Lutachuzibwa amesema,mkoa wa Mwanza unaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari Tv na radio pamoja timu za Halmashauri kuimarisha ukaguzi katika maeneo ya mipakani,bandari,uwanja wa ndege ili kukabiliana na ugonjwa huo wa Marburg.

Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt.Thomas Lutachuzibwa kwenye kikao kazi cha kutoa elimu ya kukabiliana na ugonjwa huo ambacho kimewakutanisha viongozi wa dini kutoka Jijini la Mwanza, Kamati ya Amani,Chama cha Wavuvi pamoja na Wadau mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa huo Adam Malima.

Naye Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu mkoani Mwanza Chagu Ng’homa akizungumza katika kikao hicho amesema hadi hivi sasa kila Halmashauri imeweza kuandaa eneo la kuhudumia wagonjwa watakaojitokeza kuugua ugonjwa huo zikiwemo dawa, vifaa tiba na vifaa kinga endapo watajitokeza katika mkoa huo.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Thomas Lutachuzibwa amewahasa wavuvi Mkoani Mwanza wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kupambana na virusi hatari vya ugonjwa wa Marburg uliojitekeza mkoani Kagera hivi karibuni katika maeneo ya wavuvi na kuuwa wavuvi watano.


Post a Comment

0 Comments