Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MKOANI MWANZA






Na Sheila Katikula,Mwanza

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Mitaji ya Umma,Vuma Augustine amesema, kamati hiyo imeridhishwa na Uwekezaji katika kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Amesema, wametembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo Mansipaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwani mradi huo unatija hivyo wanaipongeza Wizara ya 

Madini kwa kufanya kazi nzuri ya kulea Shirika la Madini Tanzania ( STAMICO )

Naye Waziri wa Madini Dk Dotto Biteko amesema amepokea ushauri kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Mitaji ya Umma ya iliyoagiza ikimtaka kuhakilisha Madini yote ya dhahabu yanayochimbwa nchini yasafishwe kabla ya kutoka na kwenda nje ya nchi.

Kiwanda hicho ambacho kimegharimu zaidi ya sh bilioni 16 ambacho kina ubia na Serikali ambayo inamiliki hisa ya asilimia 20.


Post a Comment

0 Comments