Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE TPA TANGA YAADHIMISHA KWA KUTEMBELEA NA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA.

Umoja wa Wanawake wa Bandari Mkoa wa Tanga wakiwa pamoja na watoto wa kituo cha Casa Della Gioia kilichopo mtaa wa Raskazoni jijini Tanga.
Wanawake hao wakiwa na zawadi mbalimbali walizowapelwkea watoto hao.
Ofisa idara ya rasilimali watu na utawala Bandari ya Tanga akikabidhi baadhi ya vitu kwa Msimamizi na mlezi wa kituo hicho Sista Consolatha Mgumba.
Katibu wa Wanawake Bandari Mkoa wa Tanga Nancy Gerald akiongea na waandishi wa habari.

Wanawake wakishusha mizigo kwenye kabla ya kuikabidhi.


**********************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

ILI kutikomeza unyajyasaji na ukatili kwa wanawake, imeshuriwa wanawake kuacha tabia ya kujibweteka badala yake wasimame wawe imara na wenye kujitambua kwa kujitafutia shuhuli itakayowaingizia kipato na kujikwamua kiuchumi.


Hayo yameelezwa na Ofisa idara ya rasilimali watu na utawala Bandari ya Tanga Sharifa Nuhu walipotembelea kutoa msaada ya vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto Casa Della Gioia, jijini Tanga ambapo alitoa wito kwa wanawake kuamka na kujitambua.


Nuhu amebainisha kwamba wanaume wengi huwafanyia ukatili wanawake ambao wamekuwa tegezi kwao kwa kuona kuwa hawezi kuchukua hatua yoyote kwa udhaifu wao.


"Sasa hivi kuna wimbi kubwa la unyajyasaji wa kijinsia kwa wanawake na hii inatokana na uwezo wao mdogo katika nyanja mbalimbali, lakini kubwa ambalo tunatakiwa kufanya, wanawake tujitume na kujikwamua kiuchumi,


"Sio lazima wote kuajiriwa, kuna kazi nyingi mbalimbali kama vile kufanya biashara, wapo wakina mama wameamka tunaiona wanapika vyakula wanajipatia kipato, na tukishakuwa na nguvu ya kiuchumi hawa wanaume watatuheshimu, na huu unyajyasaji utaisha,


"Wanaume wengi huwafanyia ukatili wanawake ambao wamekuwa tegezi kwao kwa kuona kuwa hawana kipato na hawezi kujitegemea, hivyo nitoe wito kwa wanawake wenzangu tuamke, tujitume na kujitunza ili tuwe na kipato na hili litamaliza suala zima la unyajyasaji na ukatili kwetu " amesema Nuhu.


Naye Katibu wa Wanawake Bandari ya Tanga Nancy Gerald amesema wametoa msaada katika kituo hicho kwa kuwasaidia watoto ikiwa ni kumuunga mkono Rais Samia Sulluhu Hassan katika harakati za kumlinda na kumthamini mtoto hivyo siku hii ni muhimu kwao katika kutekeleza majukumu yako.


"Wanawake sisi ni jeshi kubwa, tuna ari na tunaweza kama hivi nchi yetu inaongozwa na mama yetu Rais Samia Sulluhu Hassan, hivyo na sisi tunapaswa kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa weledi na kuleta matokeo katika maeneo yetu ya kazi" amebainisha.


Aidha amefafanua kwamba wanawake wanapaswa kuwa wa kwanza kusema vitendo viovu wanavyofanyiwa na waume lakini pia kuwalinda watoto wao siku zote kwani wao ni walinzi katika jamii ili kuepusha vitendo vya ukatili na unyanyasaji.


"Wanawake tunapofanyiwa vitendo viovu ndani ya nyumba tutoke nje, na pia tuwalinde watoto wetu, sisi tumepewa dhamana ya ulinzi kwao, na kama tukinyamaza kimya hakuna kitakachobadilika na huu ukatili hauwezi kuisha" amebainisha.


Kwa upande wake Mlezi na Msimamizi wa kituo hicho Sista Consolatha Mgumba ameushukuru umoja huo wa Wanawake wa Bandari ya Tanga kwa kuwakumbuka na kuwapelekea msaada huo kwani utawasaidia katika rika zote za watoto walio kituoni hapo kwa maana wakubwa na wadogo.


Almesema kituo hicho wapo watoto wapatao 70 wenye rika tofauti kuanzia miezi 8 hadi miaka 20 na wanapata mahitaji yao muhimu na waliofikia umri wa kwenda shule wanaendelea na masomo yao.


"Niwashukuru sana kwa kutuletea msaada huu, mnatutia nguvu sana sisi tunaowalea hawa watoto ambao wamepita misukosuko baada ya kuacha na wazazi wao, kwa maana mama anapopitia mambo ya magumu anayekuja kutaabika mbeleni ni mtoto" amesema Mgumba.


Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuweza kutumia msemo wa zamani kwamba mtoto wa mwenzako ni wako na kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kupunguza makazi ya watoto lakini pia watoto wa mitaani.


"Tunawalea hawa watoto lakini inaonesha kama hatujawanyanyua bado kwani kuongezeka watoto kwenye makazi ya kulelea inaonekana wazi kuna kitu hakiko sawa, hivyo tutumie msemo wa zamani ili kuweza kuwasaidia na kaliza tatizo hili" amebainisha.

Post a Comment

0 Comments