Ticker

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UVUNAJI SUMU YA NYUKI******************

Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya kuuza Sumu ya nyuki nchini, kutokana na uwepo wa soko kubwa Duniani na kununuliwa kwa bei kubwa.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, wakati akiwasilisha mada katika semina ya waandishi wa Habari iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), mtafiti na Mbunifu wa Teknolojia ya Uvunaji sumu ya Nyuki Patrick Kitosi, amesema sumu ya nyuki inafaida nyingi ikiwemo kutibu magonjwa mbalimbali, na ndio maana huuzwa kwa gharama.

Akizungumzia juu ya bei ya sumu ya nyuki amesema, gramu moja inauzwa kwa wastani wa shilingi laki 1.5 mpka laki tatu kwa soko la nje ya nchi, huku maeneo mengine ikiuzwa kwa laki nne.

Aidha amebainisha kuwa Soko la sumu ya nyuki lipo zaidi katika nchi za India, China, Marekani na nchi nyingine ambazo zinatengeneza dawa. Kwa mujibu wa Kitosi sumu ya nyuki inafanyia utafiti katika kutibu magonjwa ya saratani na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Post a Comment

0 Comments