Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA ELIMU YATOA SH.MILIONI 50 KWA WATAFITI

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.


SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akizindua Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' hafla iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezindua tuzo kwa wahadhiri wa elimu ya juu ambao tafiti zao zitachapishwa katika majarida ya juu ambapo chapisho litakalokidhi vigezo na kushinda litapata Sh milioni 5o.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Machi 26,2023 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals'.

Prof Mkenda amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na kuimarisha uwezo wa nchi katika kufanya tafiti na ubunifu unaolenga kuchagiza maendeleo ya uchumi wa viwanda na kuboresha maendeleo ya watanzania.

Amesema juhudi hizi zinajumuisha, pamoja na masuala mengine, kuongeza fedha na kujenga miundombinu ya kisasa ya utafiti na ubunifu sambamba na kuongeza idadi ya rasilimali watu yenye weledi stahiki na morali.

“Katika kuimarisha juhudi hizo na kuhakikisha kwamba nchi yetu inazalisha matokeo ya utafiti yanayoakisi na kujibu changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi na yenye hadhi ya kimataifa.

“Wizara imeanzisha Tuzo ya kila mwaka kwa watafiti kutoka Taasisi za Elimu ya Juu za Umma na Binafsi nchini wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hadhi ya kimataifa `High Impact Factor Journals`,”amesema Prof Mkenda.

Prof Mkenda amesema upatikanaji wa washindi wa tuzo hiyo utazingatia utaratibu na vigezo vilivyoainishwa katika mwongozo wa Kitaifa ambao umezinduliwa na kuanza kutumika rasmi kushindanisha machapisho yaliyochapishwa ndani ya kipindi cha kuanzia Juni 1 2022 hadi Mei 31 mwaka huu.

“Tuzo hii itaanza kutolewa kwa machapisho katika fani za Sayansi Asilia na Hisabati na Tiba,”amesema

Aidha,Mkenda amesema tuzo hiyo itajumuisha cheti na fedha taslimu Shilingi Milioni 50 kwa kila chapisho litakalokidhi vigezo na kushinda.

Vilevile, tuzo hiyo itatolewa kwa machapisho yote yanayokidhi vigezo kwa mwaka husika kwa kuzingatia uwezo wa kibajeti. Amesema kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni moja. Amesema wahadhiri watakaohusika na tuzo hiyo ni wale waliofanya utafiti kwenye maeneo ya sayansi asilia, hisabati na tiba na matokeo ya tafiti zao kuchapishwa katika majarida ya juu ya kimataifa.

Prof Mkenda amesema kwa kawaida matokeo ya mtafiti yatachapishwa katika majarida hayo kama dunia itayatambua na kuona kuwa mtafiti amesogeza uelewa wa binadamu katika maeneo ya sayansi na tiba.

Amesema majarida yenye hadhi ya kimataifa yatachanguliwa kwa kwa kuzingatia kigezo cha “Impact Factor”ambacho kinachoakisi ubora wa machapisho katika Jarida husika.

“Mwombaji lazima awe Mtanzania kutoka katika Taasisi yoyote ya Elimu ya Juu iliyothibitishwa na mamlaka husika nchini mathalan TCU na NACTVET.

“Kila chapisho linalokidhi vigezo na kushinda litapokea Tuzo moja pekee inayojumuisha cheti na shilingi milioni 50; na ikiwa litakuwa limehusisha waandishi wa kitanzania zaidi ya mmoja, kiasi hicho cha fedha kitagawanywa kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika Mwongozo wa Tuzo

“Mchakato wa kupata washindi utasimamiwa na Kamati ya Tuzo ambayo itateuliwa na Wizara kwa kuzingatia vigezo na uwiano ulioainishwa katika Mwongozo wa Tuzo,”amesema Prof Mkenda.

Post a Comment

0 Comments