Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAKABIDHI TIKETI THELASINI ELFU KWA TFF ILI MASHABIKI WAIONE STARS DHIDI YA UGANDA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakub (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa shughuli ya kukabidhi tiketi za mechi ya kufudhu mashindano ya mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) mapema hii leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, kulia ni rais wa shirikisho hilo Wallace Karia na kushoto ni Afisa Habari wa shirikisho hilo Clifford Ndimbo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakub (katikati) akimkabidhi rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Wallace Karia tiketi za mechi ya kufudhu mashindano ya mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda mapema hii leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari wa shirikisho hilo Clifford Ndimbo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakub (katikati) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) tiketi za mechi ya kufudhu mashindano ya mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda wakati akikabidhi tiketi hizo kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) mapema hii leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam, kulia ni rais wa shirikisho hilo Wallace Karia na kushoto ni Afisa Habari wa shirikisho hilo Clifford Ndimbo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Wallace Karia (katikati) akitoa neon la shukrani kwa serikali kwa kuweza kulipatia shirikisho hilo jumla ya tiketi thelasini elfu kwa ajili ya mashabiki kwenda kushuhudia mechi ya kufudhu mashindano ya mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakub na kushoto ni Afisa Habari wa shirikisho hilo Clifford Ndimbo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakub (hayupo pichanii) wakati wa shughuli ya kukabidhi tiketi za mechi ya kufudhu mashindano ya mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) mapema hii leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Picha na Eliphace Marwa – WUSM – Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments