Ticker

6/recent/ticker-posts

ACT WAZALENDO YALISHAURI BUNGE KUUNDA KAMATI TEULE KUFANYA UCHUNGUZI MASUALA 3 YALIYOIBULIWA NA CAG


Na Magrethy Katengu

Chama ACT Wazalendo kimelishauri Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Kamati Teule ya Bunge kufanya uchunguzi wa kina wa masuala haya matatu yaliyoibuliwa na CAG katika taarifa yake ya mwaka huu ambapo inaonesha kuna ubadhilifu mkubawa wa fedha na wahusika wote washughulikwe ipasavyo ikiwemo kutenguliwa uteuzi wao na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe wakati akichambua ripoti iliyosomwa 

Aprili 06,2023 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere taarifa yake ya Ukaguzi wa Mapato na Matumizi ya Fedha za Umma kwa mwaka wa fedha wa 2021/22 Bungeni baada ya kuikabidhi kwa Rais mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu

Zitto Kabwe akichambua kuhusu deni la Taifa amesema CAG amefanya ukaguzi wa Akaunti ya Deni la Taifa na kueleza kwamba hadi Juni 30, 2022 lilikuwa Shilingi trilioni 71 ambapo ni ongezeko la 11% kutoka deni la shilingi trilioni 64.5 lililo ripotiwa mwaka 2020/21 Uchambuzi wao unaotokana na Ripoti ya CAG unaonyesha kuwa katika mwaka huu wa ukaguzi Serikali ilichukua mikopo ya ndani kwa 30% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na mikopo ya nje yenye masharti nafuu iliyochukuliwa na Serikali ilikuwa 33% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge Mwenendo huounaonyesha Serikali kutojali na kudharau mamlaka ya Bunge hivyo wameiomba Serikali kuheshimu Bunge na kufuata sheria ya Bajeti.

Zitto amesema kuwa CAG amebainisha katika ripoti yake ya ukaguzi kuwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ilishindwa kutekeleza bajeti yake yote ya mwaka 2021/2022 licha ya kutengewa na Bunge bajeti ya shilingi trilioni 2.9.hivyo wanapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe; Moja, baada ya CAG kuthibitisha kuwa Shirika la ndege ATCL limekuwa likijiendesha kwa hasara ikiwemo kukodisha ndege kutoka TGFACAG ameonyesha, hasara na hoja kadhaa za ukaguzi zinazohusu Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). 

"Ni kweli CAG ameonyesha kuwa mwaka 2021/22, ATCL walipata hasara ya shilingi bilioni 35 kutoka hasara ya shilingi bilioni 36 ya mwaka 2020/21. Uchambuzi wetu unaonyesha kwamba hasara inayopata ATCL kwa sehemu kubwa inatokana na mfumo wa umiliki wa ndege Mfumo uliopo sasa ATCL haimiliki ndege. Ndege zote zilizonunuliwa na Serikali kwa fedha za walipa kodi zinamilikiwa na TGFA na kukodishwa kwa ATCL. Tunapendekeza ATCL imilikishwe ndege zote inazokodishiwa kutoka TGFA"amesema Zitto

Zitto aliendea kuchambua kwa kusema kuwa Katika Ripoti ya Mwaka 2021/2022, CAG ametoa hoja mbili kubwa za ukaguzi kuhusu Mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya Mabasi ya Mwendokasi Dar es Salaam (DART); ujenzi kutokidhi ubora wa viwango na matumizi ya dizeli badala ya gesi kwenye mabasi ya mradi huo.Kuhusu eneo la dizeli, CAG amebaini kuwa TPDC imeingia gharama ya ujenzi wa miundombinu kujaza gesi asilia kwenye mabasi ya mwendokasi bila ya kuwa na mkataba na DART.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa CAG, DART waligoma kuingia mkataba na TPDC kwa ajili ya kubadilisha magari kutoka mfumo wa mafuta kwenda gesi kwa madai kuwa wameingia mkataba wa miaka 12 na kampuni ya kuuza mafuta ya dizeli hivyo hoja hiyo ya mkataba wa miaka 12 haina mashiko na ni kichaka cha ubadhilifu.

"Taarifa tulizonazo zinaonyesha kwamba DART wanatumia wastani wa lita 30,000 za diseli kuendesha huduma ya usafiri kwa siku hii ni sawa na kutumia Shilingi milioni 91 kila Siku, sawa na shilingi bilioni 33 kwa mwaka mzima. ACT Wazalendo tunaitaka DART kuingia mkataba mara moja na TPDC kubadilisha mabasi ya mwendokasi kutoka kutumia Diseli na kutumia gesi asilia (CNG)Ili kuipunguzia gharama serikali "amesema Mwenyekiti

Sambamba na hayo Zitto akichambu ripoti hiyo kuhusu mikopo amesema masharti ya mkopo kutoka Benki ya Standard Chartered ya Uingereza kwenda kwa Serikali, kuongezeka kwa gharama za ujenzi wa SGR kipande cha 3 na 4 na kuongezeka kwa gharama za ununuzi wa vichwa na mabehewa ya treni ya SGR katika hali isiyokuwa ya kawaida, Serikali ilipokea mkopo kutoka Standard Chartered wenye masharti ambayo yalisababisha gharama za ujenzi kuongezeka kwa shilingi trilioni 1.7. Gharama za ujenzi kwa kipande cha 3 na 4 ziliongezeka kwa kiasi cha dola milioni 1.3 na milioni 1.6

Awali Waziri Mkuu kivuli chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu akichambua Ripoti ya CAG amesema kumekuwa na Upotevu usiokwisha wa Mabilioni ya Fedha za Mikopo kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu zinazotolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Ripoti hii imeibua hoja zenye thamani ya Shilingi Bilioni 97.59 mikopo hiyo ACT Wazalendo wanapendekeza kuwa Mikopo itolewe kupitia Skimu ya Hifadhi ya Jamii ambapo fedha hizo zitakuwa ni mchango wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wananchi wenye sifa watakaoingia kwenye Skimu husika. 

Amesema tukitekeleza mfumo huu kwa miaka mitano tutakuwa tumejenga Skimu ya Hifadhi ya Jamii yenye thamani ya shilingi trilioni 2.1 yenye wanachama zaidi ya milioni 3 wenye Fao la Matibabu. 

Semu amesema kuna Hatari ya Mfuko wa Bima ya Afya Ripoti ya CAG imebaini matatizo makubwa kwenye Mfuko wa Bima ya Afya CAG kwa mara nyingine tena ameonyesha kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaendelea kupata hasara ambapo katika mwaka huu wa ukaguzi, 2021/2022, hasara ilikuwa shilingi bilioni 205. Ikumbukwe kuwa mfuko ulipata hasara ya shilingi bilioni 104 mwaka 2020/21, hivyo hasara imeongezeka maradufu.

"CAG amebaini yafuatayo kuhusu NHIF. Kwanza wafanyakazi wamejikopesha na kusuasua kulipa kiasi cha shilingi bilioni 41.42. yaani watu wanachangia fedha mfuko halafu wafanyakazi wake wanatumia fedha hizo kujikopesha kufanyia mambo yao mengine.Kwa mwenendo huu, ni wazi mfuko wa NHIF unakwenda kufa katika muda mfupi" 

Waziri Mkuu kivuli Semu amesema Kuunusuru mfuko huo ACT imependekeza mambo mawili; Mosi kubadilishwa kwa Bodi na Menejimenti ya NHIF ambapo vyombo hivyo havina mbinu mbadala za kuendeleza mfuko huo na kubadilishwa kwa sheria nzima ya Bima ya Afya, na pili ni kuunganishwa kwa mfumo wa Bima ya Afya na ule wa Hifadhi ya Jamii kama ambavyo tumekuwa tukipendekeza.


Post a Comment

0 Comments