Ticker

6/recent/ticker-posts

BETWAY KUKUZA SOKA LA TANZANIA KUANZIA NGAZI YA MTAA

Wabishi FC kutoka Tegeta, Dar es Salaam ambao ni washindi wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mbuzi wakipokea mbuzi wawili kutoka kwa wawakilishi wa Betway Tanzania.
***

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya kimataifa, Betway Tanzania imezindua rasmi programu ya kutoa vifaa vya michezo kwa timu za soka za mtaani. Programu hiyo yenye lengo la kusaidia maendeleo ya michezo nchini Tanzania kwa kutoa vifaa kwa timu za soka ngazi ya chini itashuhudia timu za mtaani zikikabidhiwa mipira, jezi pamoja na soksi. Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo timu hizo zitashindana katika michezo ya ‘Kombe la Mbuzi’ ambayo pia imeandaliwa na Betway Tanzania kama sehemu ya programu hiyo. 


Zoezi la ugawaji wa vifaa vya michezo limezinduliwa jijini Dar es Salaam Machi 31, 2022 ambapo timu mbili kutoka wilaya ya Kinondoni zimeshakabidhiwa jezi na kuingia kwenye mashindano ya Kombe la Mbuzi ambapo timu iliyoibuka mshindi imepata mbuzi wawili na mshindi wa pili amepata mbuzi mmoja. 

 

Afisa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe amebainisha kuwa uamuzi wa kampuni hiyo kuangazia soka la mtaani ni sehemu ya Betway Tanzania kutoa mchango wake kwa jamii na kuchangia katika kukuza maendeleo ya sekta ya michezo nchini Tanzania. 

 

"Programu hii inaitwa Kits for Africa katika ngazi ya bara la Afrika. Katika programu hii Betway inatoa vifaa kwa timu za mtaani ili kusisimua michezo katika ngazi ya chini kabisa kwani huko ndiko ambako vipaji vinakozaliwa. Kwa hapa Tanzania, programu hii pia itakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya michezo katika ngazi za mitaa. Tumeamua kwenda kufanya zoeozi la kugawa vifaa katika vibanda vya kuonesha michezo maarufu kama vibanda umiza na kufanya mashindano ya Kombe la Mbuzi katika viwanja vya mtaani kabisa ili kugusa vipaji vya mtaani moja kwa moja.” Amesema Masaoe. 


Masaoe amoengeza kwamba anaamini hatua hiyo itaongeza motisha pamoja na kuwaunganisha zaidi wanamichezo na mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu hivyo kuamsha ari ya maendeleo ya mchezo huo. 


Uzinduzi wa prgramu hii umefanyika kata ya Tegeta, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo timu mbili zilipata vifaa vya michezo pamoja na kushinda mbuzi. Timu ya Wabishi FC kutoka Tegeta na Geneva FC kutoka Bunju ndizo timu za kwanza kunufaika na programu hiyo. Baada ya kupokea vifaa vya michezo timu hizo zilichuana kwenye mchezo uliofanyika Aprili 2, 2023 katika uwanja wa Tabata Shule ambapo Wabishi FC wakiibuka washindi kwa kuwafunga Geneva FC 2-1. 

 

Nahodha wa Wabishi FC, Selemani Agustin aam,eipongeza Betway Tanzania kwa mpango wake huo, na kusema kuwa itawahimiza watu wengi zaidi kushiriki katika shughuli za michezo na kuwasaidia kuimarisha afya na kuibua vipaji kwa maendeleo ya michezo ya Tanzania.  


"Huu ni mpango mzuri unaowaunganisha wapenda michezo katika ngazi za mitaa na kuhamasisha watu wengi zaidi kushiriki katika michezo. Wakati mwingine, timu yetu inashindwa kuingia kwenye mashindano mbalimbali kutokana na ukosefu wa vifaa vya michezo, hivyo msaada huu kutoka kwa Betway ni muhimu sana kwetu."

 

Mpango huo utaendelea kutekelezwa katika wilaya nyingine za Dar es Salaam na mikoa mingine ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments