Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. NCHEMBA AIAHIDI JUMUIYA YA KIMATAIFA KUWA SERIKALI ITAONGEZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kulia, akizungumza wakati wa mdahalo wa viongozi wa juu wa nchi za Afrika, kuhusu chakula na kilimo, ulioandaliwa na Taasisi inayojihusisha na uhamasishaji wa masuala ya kilimo Barani Afrika (AGRA), jijini Washington D.C, Marekani, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kuwekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuifanya nchi kuwa ghala la chakula Afrika na duniani kwa ujumla.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika picha na Rais wa AGRA Bi. Agnes Akalibata, baada yakumalizika kwa mdahalo wa viongozi wa juu wa nchi za Afrika, kuhusu chakula na kilimo, ulioandaliwa na Taasisi inayojihusisha na uhamasishaji wa masuala ya kilimo Barani Afrika (AGRA), jijini Washington D.C, Marekani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGRA, ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Dessalegn akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), baada ya kutoa mada kuhusu maendeleo ya sekta ya kilimo Barani Afrika na changamoto zake, mada iliyowagusa wadau wengi, ukiwahusisha viongozi wa juu wa nchi za Afrika, kuhusu chakula na kilimo, ulioandaliwa na Taasisi inayojihusisha na uhamasishaji kilimo Barani Afrika (AGRA), jijini Washington D.C, Marekani.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGRA, Mhe. Hailemariam Dessalegn (kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, na Balozi wa Tanzania-Marekani, Dkt. Elsie Kanza, wakifuatilia mjadala kuhusu chakula na usalama wa chakula, wakati wa mdahalo ulioandaliwa na AGRA na kuwahusisha viongozi waandamizi Barani Afrika, jijini Washington D.C, Marekani.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Washington D.C)

Post a Comment

0 Comments