Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII YASHAURIWA KUACHA KUTEGEMEA ULEZI KINA MAMA

-Mwenyekiti wa Taasisi ya kiraia Majlis Al-Maarifa Tahir Khatib Tahir akimkabidhi vyakula kwa ajili ya futari Zainab Seif Ali ambae ametelekezwa na mume wake akiwa na mtoto mwenye ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo huko Welezo Zanzibar wakati wa ziara yao ya ugawaji wa futari kwa wajane, walio na watoto mayatima na wasiojiweza. 07.04.2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Mama alietelekezwa na mume wake kwa kuwa na mtoto mwenye ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo Zainab Seif Ali alipokuwa akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Suhaila wakati alipotembelewa na Taasisi ya Majlis Al-Maarifa Islamiya na kukabidhiwa vyakula mbalimbali kwaajili ya futari huko Welezo Zanzibar. 07.04.2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Mwenyekiti wa Taasisi ya kiraia Majlis Al-Maarifa Islamiya Tahir Khatib Tahir akimkabidhi vyakula kwa ajili ya futari Ali Sheha Shaame anaeishi katika Mazingira magumu huko Mtoni Kidatu. 07.04.2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.


***********************

Na Fauzia Mussa,Maelezo Zanzibar 07.04.2023


Jamii imeshauriwa kutokuwaachia ulezi akina mama Peke Yao pale wanapo baini wamejifungua watoto wenye matatizo ya kiafya kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na matakwa ya dini .

Imeelezwa kuwa kuna baadhi ya kina Baba hutelekeza nyumba zao kwa kukwepa gharama za matibabu ya watoto wao na kuwachia jukumu kubwa akina mama.

Akikabidhiwa msaada wa vyakula mbali mbali kwa ajili ya futari kutoka kwa Taasisi ya Majlis al-maarif huko Welezo bi Zainab seif Ali ambae ni mama wa mtoto abuubakar mwenye ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo aliekimbiwa na mume wake amesema amekuwa akipata shida kumhangaikia mtoto huyo kutokana na gharama za matibabu yake kuwa kubwa.

" Tangu nilivyo mzaa mtoto huyu hadi sasa mtoto hamjuwi Baba yake wala Baba hamjuwi mwanawe. Siku za mwanzo mkwe wangu alikua ananisaidia lakini kunisaidia kwakwe nikimuambia naenda Hospitali ananiachia elfu kumi Tu ambayo haikidhi haja ya mtoto huyo kutokana na gharama za matibabu yake kuwa juuu",alisema mama wa mtoto huyo

Aidha amefahamisha kuwa gharama za matibabu ya mtoto huyo ni kubwa na Kila mwezi hulazimika kurudishwa hospitali kufanyiwa vipimo kutokana na ugonjwa alio kuwa nao,hivyo amewaomba wahisani kujitokeza kumsadia kwani Hadi sasa Taasisi ya Majlis pekee ndio imejitokeza kumsadia mtoto huyo katika matibabu.

Mama huyo alifafanua kuwa mtoto wake amefikia umri wa miaka sita lakini bado anahudumiwa kama mtoto mchanga hivyo ana uhitaji wa vitu mbalimbali kama vile sabuni na pempasi .

Mapema mama Abuu aliwaasa kina baba kushirikiana kwa pamoja katika malezi na kuwa na Imani na huruma kwa watoto wao hasa wagonjwa na wenye ulemavu

“Nilimzaa akiwa mzima kufika miezi sita alipata homa ya kukutwa, nikatibu spitali na na nyumbani bila mafanikio akiwa na miaka miwili ndio aligunduliwa na ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo , ni miaka sita nimekua nikimlea mwanangu Abuubakar bila ya mashirikiano yoyote kutoka kwa upande wa Baba yake ,mara tu baada ya mwanangu kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo Babake alinikimbia”kwahisia alielezea mama huyo

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya kiraia Majlis Al-Maarifa amewataka watu wenye uwezo kuwasaidia wasiojiweza ili kuweka usawa wa upatakinaji wa mahitaji ikiwemo futari katika mwezi mtukufu wa Ramadhan .

Aidha alisema kuwa Taasisi ya Majlis imeamua kwenda nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha sadaka zao zinafika sehemu husika na kwa watu husika kwani kuna baadhi ya misaada huwa haiwafikii walengwa .

Nao wanufaika wa msaada huo wameishukuru Tasisi ya Majlis Al-Maarifa kwa kuwapatia vyakula mbalimbali vitakavyowasaidia katika futari na kuwataka wengine wenye uwezo kuiga mfano wa taasisi hio kwa kwenda nyumba kwa nyumba kwani baadhi ya wanaopewa misaada hiyo huwa hawaifikishi 


Jumla ya familia 189 za maeneo mbalimbali ya Unguja zimenufaika na vyakula mbali mbali kwaajili ya futari ikiwemo unga wa ngano,sukari,mafuta na mchele kutoka kwa Taasisi ya Majlis Iliyopo Welezo.

Post a Comment

0 Comments