Ticker

6/recent/ticker-posts

KINANA AHITIMISHA MAFUNZO YA VIONGOZI VIJANA KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo ya muda mfupi ya uongozi kwa vijana 74 wanaotoka katika vyama Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha afrika kusini, SWAPO Cha Namibia, ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA Cha Angola. (PICHA NA FAHADI SIRAJI)


Washiriki wa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi wakisikiliza hotuba ya Ufungaji Vijana hao wanaotoka katika vyama Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha afrika kusini, SWAPO Cha Namibia, ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA Cha Angola.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana akigawa Vyeti kwa Wahiriki wa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi wanaotoka katika vyama Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha afrika kusini, SWAPO Cha Namibia, ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA Cha Angola.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Anamringi Macha wakati wa kufunga mafunzo ya muda mfupi ya uongozi kwa vijana 74 wanaotoka katika vyama Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha afrika kusini, SWAPO Cha Namibia, ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA Cha Angola. (PICHA NA FAHADI SIRAJI)

Washiriki wa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi Wakiimba nyimbo wakati wa Ufungaji wa mafunzo ya Vijana hao wanaotoka katika vyama Vyenye Ushirikiano wa Pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambavyo ni ANC Cha afrika kusini, SWAPO Cha Namibia, ZANU- PF Cha Zimbabwe, FRELIMO Cha Msumbiji na MPLA Cha Angola. (PICHA NA FAHADI SIRAJI)

***********************


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,ametoa rai kwa vyama sita vilivyoshiriki katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika kuendelea kuwapa mafunzo viongozi vijana kwa lengo la kuwaandaa wawe bora kwa ustawi wa vyama na mataifa yao kwa ujumla.


Amesema anaamini vijana wakipata mafunzo yatawaanda kushika uongozi katika sekta mbalimbali za mataifa yao na yatawasaidia kuongeza uwelewa na kuleta matokeo chanya.


Kinana aliyasema hayo jana wakati akifunga programu ya mafunzo kwa viongozi vijana, kutoka vyama sita vya wapigania uhuru nchi za kusini mwa Afrika.


“Kazi ya kuwalea vijana ni pamoja na kuwafunza, kuwasamehe pale wanapokosea , kuwasahihisha ili wapate taaluma ya uongozi na kuwa viongozi bora wa kuongoza wananchi wa nchi zetu.


“Tuache kutumia lugha kuwa vijana ni taifa la kesho, vijana sio taifa la kesho, vijana ni viongozi wa leo lazima tuwape nafasi ya kuongoza,”alisema


Alisema asilimia 70 ya Watanzania na nchi nyingi Afrika ni vijana na ni viongozi wa sasa hivyo ni vyema waaminiwe na kupatiwa nafasi ya kuongoza.


Pia Kinana alishukuru Chama Cha Kikomonisti cha China (CPC) kwa kuendelea ushirikishiana na vyama hivyo, huku akisema CCM itaendelea kudumisha umoja na ushirikiano baina ya vyama it it vyote.


Vyama vilivyoshiriki katika katika mafunzo hayo CCM kutoka Tanzania, SWAPO kutoka Namibia, MPLA kutoka Angola, ZANU PF kutoka Zimbabwe , ANC Afrika Kusini na FRELIMO kutoka Msumbiji.

Post a Comment

0 Comments