Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU JAMAL KATUNDU AONGOZA KIKAO CHA USHIRIKIANO BAINA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA WIZARA YA KAZI KENYA


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akiongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya walipotembelea Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), jijini Dar es Salaam tarehe 18 Aprili, 2023.

Baadhi ya wajumbe kutoka Wizara ya Kazi nchini Kenya wakifuatilia majadiliano hayo yaliyolenga kubadilishana uzoefu katika masuala ya yanayohusu sekta ya kazi na ajira walipotembelea Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), jijini Dar es Salaam tarehe 18 Aprili, 2023.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi, Bi. Hadija Mwenda akifafanua jambo wakati wa kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya, jijini Dar es Salaam tarehe 18 Aprili, 2023. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu.


Kaimu Meneja wa Usalama (OSHA), Mhandisi Robert Mashinji akitoa mada kuhusu masuala ya Usalama mahala pa kazi wakati wa kikao hicho.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko pamoja na watendaji walioambatana nao wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao hicho.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu (wa pili kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko (wa pili kutoka kulia) pamoja na watendaji kutoka Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA), Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) na wajumbe kutoka Wizara ya Kazi nchini Kenya.



Mkurugenzi wa Huduma za Ajira (TaESA) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Joseph Nganga akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko pamoja na watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala ya ukuzaji ajira kwa wakati ugeni huo ulipotembelea Ofisi ya TaESA, jijini Dar es Salaam.



PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

*********************

Na; OWM – KVAU: DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu ameongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhamaji nguvu kazi, ukuzaji ujuzi kwa vijana, ukuzaji ajira na masuala mengineyo yanayohusu sekta ya kazi na ajira.


Akizungumza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema kuwa kikao hicho cha majadiliano kitafungua fursa kwa nchi hizo kushirikiana kwa karibu katika kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa majukumu sambamba na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko amepongeza namna ambavyo Ofisi ya Waziri Mkuu katika kukuza fursa za ajira, viwango vya kazi sambamba na kusimamia usalama na afya kwa wafanyakazi.

Aidha, Ujumbe huo umetembelea ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja na Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA).

Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko anayesimamia masuala ya Kazi nchini Kenya.


Post a Comment

0 Comments