Ticker

6/recent/ticker-posts

MOROGORO IPO TAYARI KWA SHEREHE ZA MEI MOSI, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati amevaa batiki) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa (amevaa kofia nyeupe) wakikagua Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambao utatumika kwa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi 2023 mkoani humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (amevaa batiki) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa (amevaa kofia nyeupe) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Jamhuri Morogoro Aprili 20, 2023 Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi (wa kwanza kushoto) akielezea maendeleo ya mashindano way a Mei Mosi yanayoendelea mkoani Morogoro. Wa katikati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (ameskilikia mpira) na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa (amevaa kofia nyeupe).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (amevaa batiki) akikagua timu ya mpira wa miguu ya TANESCO kabla ya kuanza kwa mtanange Aprili 20, 2023 mkoani Morogoro. wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa (amevaa kofia nyeupe).

Baadhi ya wanamichezo wakiapa wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

*********************

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo mkoa huo upo tayari kwa maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Kitaifa yatakayofanyika mkoani humo Mei 01, 2023.

Katika ukaguzi huo, Prof. Ndalichako aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa ambapo walitembelea viwanja vya mpira wa miguu na netiboli ambayo vipo ndani wa huwanja wa jamhuri na kukagua mazingira ya uwanja huo tayari kwa maadhimisho ya Mei Mosi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Prof. Ndalichako alipata wasaa wa kukagua timu zinazoshiriki michezo hiyo na kuwasisitiza wanamichezo kutumia fursa hiyo kufanya mazoezi na kucheza michezo kwa manufaa ya afya zao na kuongeza tija katika utendaji wao wa kazi.

Timu alizokagua ni za michezo ya kuvuta kamba wanaume, timu ya Uchukuzi imewavuta timu ya Utamaduni kwa mivuto 2-0, kamba wanawake timu ya Uchukuzi imewavuta timu ya TANROAD kwa mivuto 2-0. Katika mchezo wa mpira wa miguu matokeo yakiwemo kwenye mabano, timu ya Sekta ya Uchukuzi wamewashinda Ukaguzi (6-1); TANESCO vs Wizara ya Maliasili na Utalii, Mahakama vs Maliasili na Utalii; 21 Century vs Hazina kila mmoja (0-0); TAMISEMI vs Wizara ya Afya; Wizara ya Kilimo vs NFRA; TRA vs SUA kila mmoja (1-0); Benki ya CRDB vs TPDC (1-1); TANROADS vs RAS Dodoma; Mambo ya Ndani vs Ushirika kwa kila mmoja (2-1).

Kwa upande wa netiboli timu ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wamewafunga Benki ya CRDB kwa magoli 29-19; nao Wizara ya Mambo ya Ndani waliwafunga Wakala wa Taifa wa Hifadhiya Taifa (NFRA) kwa magoli 69-12; huku Ukaguzi waliwachapa Halmashauri ya Gairo kwa magoli 47-10; wakati Sekta ya Uchukuzi waliwaadabisha Moro DC kwa magoli 65-6.

Katika michezo mingine timu ya RAS Dodoma waliwafunga Shirika la Maendeleo ya Petrol kwa magoli 33-31; nayo Ofisi ya Rais Ikulu waliwafunga jirani zao Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa magoli 56-10; huku Mahakama waliwachapa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa 37-3; na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) waliwaliza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa magoli 45-17.

Post a Comment

0 Comments