Ticker

6/recent/ticker-posts

MTANDAO WAKWAMISHA HUDUMA ZA RITA MISSENYI


Na Shemsa Mussa, Kagera.

Wananchi wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kufuata utaratibu uliyopo wa namna ya kupata vyeti vya kuzaliwa.

Akizungumza na 'Sayari Blog' afisa wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini RITA wilaya ya Missenyi Bw Jamardin Sadick Msafiri amesema kuwa ili kupata cheti cha kuzaliwa ni lazima mwombaji afike katika ofisi hizo ili kupewa utaratibu.

"kwa sasa utaratibu uliyopo mwombaji afike ofisini achukue fomu na kufuata maelekezo yanayofuata ikiwemo ofisi ya kata ,Uhamiaji na vitambulisha vya wazazi "amesema Jamardin.

Aidha bw Msafiri ameongeza kuwa wilaya hiyo haina mfumo wa kuchukua fomu kwa njia ya mtandao kutokana wilaya hiyo kuwa mpakani na kupelekea uwepo wa mwingiliano wa watu kutoka mataifa jirani.

" kwa hiyo changamoto kubwa ni hiyo mwingiliano wa watu unajua sisi tupo mpakani tumepakana na ugandakwahiyo unaweza kuona ni mtanzania kumbe ni mganda tumetumia njia hiyo ili kudhibiti wimbi hilo la watu wasio raia wa Tanzania" Ameongeza Jamardin.

Hata hivyo afisa huyo ameitaja changamoto ya mtandao inasababisha wananchi waliokamilisha utaratibu kuchelewa kupata vyeti vyao.

Post a Comment

0 Comments