Ticker

6/recent/ticker-posts

MWANAMUZIKI HUSSEIN JUMBE AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound, amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. 

Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.

Post a Comment

0 Comments