Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT SAMIA ATOA MKONO WA EID KWA MAIMAMU, WAJANE NA YATIMA MKOANI PWANI


Na Mwamvua Mwinyi,Pwani


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Mkono wa Idd kwa Maimamu wa Misikiti, walimu wa Madrasa, Wajane na Yatima Mkoa wa Pwani .


Salaam Hhzo zimewasilishwa leo April 20.2023 na Nickson Simon Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa Niaba ya Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge.


Nickson alieleza kati ya vitu vilivyotolewa ni pamoja na mchele,sukari na fedha.


Batuli Mayelo ni Mwakilishi wa wajane alimshukuru Rais kwa alichotoa na kumuombea kwa Allah amlinde katika majukumu yake ya kuliongoza Taifa.


Sheikh Mkuu Mkoani Pwani Hamis Mtupa aliwataka wananchi kuendelea kumuombea Rais na kumuunga mkono kwa makubwa anayoyafanya nchini, kutatua kero za wananchi na kuinua maendeleo na uchumi.

Post a Comment

0 Comments