Ticker

6/recent/ticker-posts

ULEGA: VITUO ATAMIZI FURSA YA AJIRA KWA VIJANA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mizengo Pinda walipokuta katika Kongamano la Tisa la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu masuala ya sera linalofanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akitoa neno kuhusu sekta za mifugo na uvuvi katika Kongamano la Tisa la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu masuala ya sera linalofanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2023.


********************

Na Mbaraka Kambona


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema wizara yake imeanzisha vituo atamizi vya kuwafundisha vijana ufugaji wa kisasa wa mifugo na samaki lengo likiwa ni kujibu changamoto ya ajira kwa vijana.

Waziri Ulega aliyasema hayo katika Kongamano la Tisa la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu maswala ya sera linalofanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2023.

“Tunamshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuturidhia kuanzisha programu hii kwa ajili ya kuandaa vijana kufanya ufugaji wa kibiashara ambapo kwa mwaka huu tumeanzisha vituo atamizi nane vya kuwafundisha vijana ufugaji kwa tija”, alisema

Alisema kuwa kila mwaka takriban vijana 1600 wanahitimu ngazi mbalimbali za elimu katika vyuo vya mifugo na kati ya hao 150 tu ndio hupata nafasi katika mfumo rasmi wa ajira hivyo lengo la ubunifu huu tulioufanya ni kuwezesha vijana wanaobaki kujiajiri kupitia unenepeshaji na uuzji wa mifugo yake ndani nan je ya nchi.

“Mipango yetu katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 ni kuwa na vituo atamizi 30 ambavyo vitakuwa na vijana wasiopungua 30 na kutufanya kuwa na vijana 900 ambao watakuwa wamepata mafunzo hayo na kuweza kujiajiri wenyewe kupitia mitaji watakayokuwa wameipata wakati wa mafunzo hayo”,alifafanua

Aliongeza kuwa tayari wizara imeshatafuta masoko kwa ajili ya vijana hao kuuza mifugo yao ambapo kwa mwaka vijana hao watauza mifugo yao takriban mara nne kwa mwaka na hivyo kuwawezesha kupata kipato ambacho kitamsaidia akimaliza kuwa na mtaji wa kujiajiri.

Halikadhalika, aliongeza kuwa vituo atamizi hivyo wamevianzisha pia kwa upande wa sekta ya uvuvi kwa ajili ya vijana kuboresha ujuzi wa ufugaji wa samaki na uvuvi.

Kauli mbiu na dhima ya Kongamano hilo ni “Ushindani wa Tanzania Katika Soko Huru Barani Afrika (AfCFTA): Changamoto na Fursa Katika Sekta ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi.

Post a Comment

0 Comments