Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU WANNE JELA MIAKA 20 KWA KUBAINIKA NA PEMBE ZA NDOVU SHINYANGA**********************

Na Elias Gamaya, Shinyanga.

Mahakama ya hakimu mkazi shinyanga imewahukumu watu wanne kwa kosa la uhujumu uchumi kesi namba moja ya waka 2022 mara baada ya kukutwa na nyara za serikali pembe za ndovu zenye thamani ya Tshs milioni 69.21 ambapo ni kinyume cha sheria.

Akitoa hukumu huyo hakimu mkazi Yusuphu Zahoro kwa washtakiwa hao ambao ni Emmanueli Shija,Shija kaswahili aliyekuwa mtendaji wa kata ya Solwa Revocatus mtala na Daudi ndizu ambao walitenda kosa hilo julai 12,2022 walikutwa na vipande tisa za pembe za ndovu zenye thamani ya milioni 69.21 ambapo washitakiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye harakati ya kuuza nyara hizi maeneo ya kata ya Solwa wilayani Shinyanga Mkoani shinyanga.

Akizungumza nje ya mahakama muendesaha mashtaka kiongozi mkoa wa Shinyanga Jukael Jairo amesema wamewidhishwa na uamuzii uliyotolewa na mahakama kutokana na uhajumu uchumi.

Hata hivyo kabla ya hukumu washitakiwa waliimba mahakama kuwapa adhabu ndogo kwani wanaumwa Pamoja na kutegemewa na familia huku wakili wa serikali akiiomba serikali itoe adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Post a Comment

0 Comments