Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM MUHEZA WAANZA UJENZI WA JENGO JIPYA LA UTAWALA LA GHOROFA

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Like Gugu akichimba msingi jana kuashiria kuanza ujenzi wa Jengo la CCM wilaya ya Muheza la Ghorofa ambalo litajengwa eneo la Kata ya Genge wilayani humo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Like Gugu akichimba msingi kuashiria kuanza ujenzi wa Jengo la CCM wilaya ya Muheza la Ghorofa ambalo litajengwa eneo la Kata ya Genge wilayani humo

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Like Gugu akizungumza mara baada ya kumalizika halfa ya uchimbaji wa msingi kuashiria kuanza ujenzi wa Jengo la CCM wilaya ya Muheza la Ghorofa ambalo litajengwa eneo la Kata ya Genge wilayani humo

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye pia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza Desderia Haule akizungumza wakati wa halfa hiyo ambapo alikipongeza chama hicho

Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng’ese akieleza jambo katika halfa hiyo

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Muheza Herbet Mtangi akizungumza wakati wa halfa hiyo

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali

Mafundi wakiendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi huo


Na Oscar Assenga, MUHEZA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza mkoani Tanga wameanza ujenzi wa Jengo Jipya la Utawala la Ofisi za Chama hicho la ghorofa ambalo litatumika kwenye shughuli mbalimbali.

Hatua hiyo hiyo inatokana na makubaliana waliokubaliana kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya wilaya kwamba wanajenga jengo jipya la kisasa katika eneo ambalo waliachiwa na wazee.

Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa uchimbaji wa msingi wa ujenzi huo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu alisema kwamba mradi huo wa ujenzi wa jengo hilo utagharimu Milioni 260

Alisema kwamba wao kama wilaya watajitahidi kutafuta fedha kwa wahisani na kushirikiana na wanachama hao ili kuweza kufanikisha malengo ya ujenzi wa ofisini hiyo ambayo wanamatumaini itakamilika kabla yam waka 2025.

“Jengo letu la zamani tutalitumia kwa ajili ya biashara na tulikubaliana kwamba wanajenga Jengo la ofisi ya CCM wilaya kwenye kikoa cha Halmashauri kuu na kwamba wanataka kujenga la kisasa kwenye uwanja tulioachiwa na wazee kabla ya kufika m waka 2025 jengo hilo lianza kutumika”Alisema Mwenyekiti huyo

Hata hivyo alisema kwamba watashirikiana na wana CCM wilayani humo kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati kabla ya muda wa kampeni kuanza ili liweze kutumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kichama.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) Desderia Haule aliipongeza CCM kwa kubuni wao na kuanza ujenzi wa Jengo nzuri la kisasa ambalo hata hadhi ya wilaya itaonekana kwa viongozi watakaokuwa wakifika wilayani humo huku akihaidi kushirikiana nao.

Katibu Tawala huyo aambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Muheza alitoa wito kwa wana CCM wilaya ya Muheza kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kwa kujitoa ili kuweza kufanikisha ujenzi huo ili kabla ya mwaka 2025 wakati wa hekaheka za uchaguzi liwe limekamilika.

‘Pale tulipo kuwa zamani hapatoshi hivyo tukiwa hapa itakuwa nzuri sana hivyo kikubwa tuendelea kushirikiana kuweza kufanikisha ujenzi huu ambao ni muhimu”Alisema

Hata hivyo alitoa wito kwa Katibu na Mwenyekiti CCM wilaya hiyo kuendelea kupambana kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya Chama na kwamba wao kama Serikali watawaunga mkono.

Naye kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng’ese alisema chama hicho ni kikubwa na wanapaswa kuwa na jengo nzuri la utawala na kwa bahati nzuri wilaya hiyo wazee waliowatangulia walipambana kupatikana jengo hilo la utawala ambalo pembeni yake wamejenga nyumba za makatibu na wao CCM watabaki kwenye ujenzi huo wa ofisi ya wilaya.

Alisema wilaya ya Muheza ni tajiri katika mazao ya viungo wanajiona wana uwezo pia wamekusudia kujenga jengo nzuri na wamebuni kuchora ramani ya ghorofa moja ili angalau Jumuiya ziwe chini na chama juu na kuwepo kwa ukumbi kwa ajili ya vikao na wamekusudia hivyo.

“Leo tumefanya Halmashauri kuu maalumu na tumepata fedha ambayo itamalizia msingi na kutolea matoleo kwa ajili ya kuweka matofali tunashuruku ushirikiano wa Serikali ya wilaya na Mbunge wetu Naibu Waziri wa Michezo ,Sanaa na Utamaduni Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA kutuunga mkono kwenye jambo hili “

Post a Comment

0 Comments