Ticker

6/recent/ticker-posts

LHRC YAZINDUA TAARIFA YA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KWENYE HAKI ZA BINADAMU

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kutekeleza malengo a maendeleo endelevu na kuhakikisha kunakuwepo na ustawi wa vizazi vijayo, LHRC inatoa rai kwa serikali, taasisi na jamii ya Watanzania kwa umoja w e t tuchukue hatua zitakazotuwezesha kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia c h i kwa ustawi wa vizazi vijavyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt.Anna Henga wakati wa Uzinduzi wa Taarifa ya Athari za Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye Haki za Binadamu uliofanyika leo Mei 18,2023 kwa njia ya Mtandao.

Amesema Ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwenye haki za binadamu imebainisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana dhahiri kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi yakiwemo masuala ya afya, upatikanaji wa maji safi, mazingira kwa ujumla wake pia kukosekana kwa usawa, kwani wale wanaoteseka zaidi wakati wa shida ya mazingira ni watu walio hatarini (makundi maalumu).

Aidha amesema Haki ambazo zimeonekana zinaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na haki za kijamii kama vile haki ya chakula ‚haki ya afya, haki ya elimu, haki ya upatikanaji maji safi na salama, haki ya kuishi mazingira stahiki,haki ya faragha na familia.

"Haki za kiuchumi pia zimeendelea kuathiriwa na mabadiliko haya hasa kwenye sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kwani wananchi wameendelea kuathirika Zaidi kwa uwepo wa upatikanaji hafifu wa bidhaa za kilimo na uvuvi pamoja na uwepo wa magonjwa mbali mbali yanayoathiri mifugo". Amesema

Katika uapnde wa haki za kiutamaduni , amesema ripoti imebainisha wananchi kuendelea kuhama maeneo vao ya asili kutokana na kukosekana kwa chakula na maji na kushindwa kufanya shughuli za kilimo ambazo ni tegemeo kwa ustawi wao.

"Makundi maalum kama vile wanawake na watoto pia vameathiriwa kwani kwa kuhama hama Watoto wengi wameshindwa kufikia haki yao ya elimu na wazazi wameendelea kutelekeza familia kutokana na kuhama kutafuta maeneo stahiki ya kuishi". Amesema

Post a Comment

0 Comments