Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS AITEMBELEA FAMILIA YA HAYATI EDWARD SOKOINE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 19 Mei 2023 wameitembelea familia ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na familia hiyo ikiongozwa na mjane wa Hayati Sokoine Bi. Napono Sokoine ambao wamemshukuru kwa kuwatembelea kijijini hapo na kuipongeza serikali kwa jitihada mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha Makamu wa Rais na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wameweka shada la maua na kuongoza sala ya kumuombea Hayati Edward Moringe Sokoine katika kaburi lake lililopo katika eneo la nyumba hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwasili nyumbani kwa Mjane wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Bi. Napono Sokoine (Mwenye nguo nyekundu) katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala katika kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati walipofika nyumbani kwa familia ya Sokoine Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati walipofika nyumbani kwa familia ya Sokoine Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati alipofika nyumbani kwa familia ya Sokoine Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa na familia ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakiongozwa na Bi. Napono Sokoine (Mwenye nguo nyekundu) ambaye ni mjane wa Hayati Sokoine wakati alipowatembelea nyumbani kwao Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023. Wengine ni viongozi wa mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo John Mongela.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na baadhi ya wanafamilia wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakiongozwa na Bi. Napono Sokoine (Mwenye nguo nyekundu) ambaye ni mjane wa Hayati Sokoine wakati alipowatembelea nyumbani kwao Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakipokea zawadi za mavazi ya kabila la wamaasai wakati walipowasili nyumbani kwa Mjane wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine Bi. Napono Sokoine (Mwenye nguo nyekundu) katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo tarehe 19 Mei 2023.

Post a Comment

0 Comments