Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE KITANDULA ATAKA MNADA WA MIFUGO HOROHORO UFUNGULIWE



Na Mwandishi Wetu,Dodoma.


MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ameiomba Serikali kupitia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulenga kufungua mnada wa mifugo uliopo eneo la Horohoro mpakani kwa Tanzania na Kenya ili wafugaji waweze kunufaika na uwepo wake.


Kitandula aliyasema hayo wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo alisema wanaishukuru Serikali kwa kuweza kuwatatulia kilio chao cha muda mrefu cha kutokuwa na mnada wa uhakika eneo hilo na hivyo kuweza kuanzisha na sasa umekamilika.


Alisema kwamba wanaishukuru Serikali pamoja na kukamilika kwa mnada huo na wananchi kufurahia jambo hilo lakini umekuwa kero kwa sababu tangu kukamilika kwa mnada huo mwazoni mwa mwaka huu mpaka leo haujawahi kufunguliwa.


“Hivyo nikuombe Waziri wa Mifugo na Uvuvi ndugu yangu Ulega hili unaliweza nakuomba tukimaliza wizara yao kazi ya kwanza nakuomba twende tukafungue ule mnada”Alisema


Mbunge Kitandula alisema kwamba mkandarasi anakataa kukabidhi huo mnada kwa sababu anawadai karibia milioni 100 hizo wana uwezo nazo hivyo waende kufungua huo mnada kwa sababu wanapoteza fursa ya mapato.


“Kwa sababu hali ya upande wa pili ya Kenya ni mbaya kwa minada yao hivyo wakifungua watapiga bao hivyo twenda tukafanye jambo hilo kwa haraka litakuwa na tija kubwa”Alisema


Katika hatua nyengine Mbunge Kitandula alisema mwaka jana waliomba majosho 10 wamepata mawili sio haba wanaishukuru serikali kwani walipata jumla ya milioni 46 wakapeleka kibewani na mkota hivyo wanaoimba yaliyobakia wafikiriwe pale duga wana josho walilijenga tokea mwaka 1972 limechakaa nakuomba sana josho hilo ni muhimu lifanyiwe kazi kwa haraka.

Post a Comment

0 Comments