Ticker

6/recent/ticker-posts

NYUKI SAFARI YAPAMBA MAADHIMISHO YA SIKU NYUKI DUNIANI MKOANI SINGIDA, VIVUTIO VYA UTALII VYAPAA


Na.Mwandishi Wetu-SINGIDA

Programu maalumu ya kuhamasisha Utalii wa Ndani maarufu kama 'Nyuki Safari' imefana kwenye Maadhimisho ya siku ya Nyuki Duniani mkoani Singida ambapo wadau wa Misitu na Ufugaji Nyuki wametembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo mkoani humo.

Programu hiyo mahsusi imeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuhamasisha Utalii wa ndani sambamba na kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa kupitia Filamu Maarufu ya ' The Royal Tour'

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mhifadhi Historia kutoka Mkoa wa Singida, Moses Msai amesema mkoa huo umebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambapo Wadau hao wamepata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vivyopo mkoani humo ikiwemo maeneo ya Malikale.

" Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yamechagiza vivutio vya utalii vya mkoani Singida kujulikana hivyo ni imani yangu kuwa ziara hii imeacha alama kubwa" amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ufugaji Nyuki (TABEDO) Rudia Hamudu Issa aliyeshiriki ziara hiyo amesema ziara hiyo ni muhimu kwani imeutangaza mkoa wa Singida kiuwekezaji.

" Nimeifurahia sana ziara hii kwani Mimi na Wenzangu tumejifunza mengi, Singida imebarikiwa kuna vivutio vingi sana hasa vya Malikale" Amesema

" Tumeona Vivutio vya Malikale vizuri, Tumepata Historia ya Mtemi Senge Mughenyi ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa Wanyamapori Saadani, Haya ni mambo ambayo Watanzania wanatakiwa kuyafahamu na kuyaendeleza kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi cha baadae" amesema Hamudu

Katika ziara hiyo ya Wadau wametembelea maeneo mbalimbali ya vivutio ikiwemo eneo la Malikale la Bomani, eneo la Ziwa la Kitalii la Singidani, eneo la Makumbusho lililopo katika Chuo Kikuu Huria cha Singida, Jengo la Bohari ambalo kichwa cha Mwanamama aliyepigana na Wajerumani kwa kutumia Nyuki Maarufu kama Jengo la Bohari pamoja na Makazi ya Mtemi Senge Mughenyi, Kiongozi aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wakazi wa Singida kwa ujumla

Post a Comment

0 Comments