Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINYI ASHUHUDUA UTIAJI WA SAINI YA MRADI WA SEKTA YA AFYA BAINA YA CHINA NA ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa Saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,wakisaini Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui(kulia) na (kushoto) Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-5-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua Mradi wa Saratani ya Shingo ya Mlango wa Kizazi na Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dr. Li Bin, wakati wa utiaji wa Saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, jumla ya Miradi mitano imezindulia leo 16-5-2023. Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Kasha mgeni wake Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dr. Li Bin, baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji wa saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-05-2023.(Picha na Ikulu)
Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dr. Li Bin na Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng (kulia) wakipiga makofi kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza katika hafla ya utiaji wa saini ya ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-5-2023 na (kushoto) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui,Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdallah na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dr. Li Bin alizungumza katika hafla ya utiaji wa saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-5-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments