Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI WA CHWAKA KATIKA MAZIKO YA BABA MZAZI WA MKUU WA WILAYA YA MJINI UNGUJA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wa Chwaka na kutowa mkono wa pole kwa Ndugu na Jamaa wa Marehemu Simai Msaraka Pinja, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja leo 13-5-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Wananchi wa Chwaka katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Simai Msaraka Pinja, ikisomwa na Sheikh Abdalla Khamis Juma (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika Kijijini kwao Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja leo 13-5-2023 na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe. Rashid Sima Msaraka, Mtoto wa Marehemu na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Simai Msaraka Pinja, wakati wa maziko yake yaliyofanyika Kijiji kwao Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja leo 13-5-2023..(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Wananchi wa Chwaka katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Simai Msaraka Pinja, ikisomwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume.(kushoto kwa Rais) na kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja leo 13-5-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments