Ticker

6/recent/ticker-posts

TUMIENI NJIA SAHIHI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI-PROF.MSHANDETE.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Naibu Makamu Mkuu Taaluma, Utafiti na Ubunifu Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa. Antony Mshandete akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati akifungua baraza hilo 26 Mei,2023 jijini Arusha.


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Suzana Augustino akifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi wa baraza la wafanyakazi lililofanyika 26 Mei, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo.


Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia wakiimbi wimbo wa mshikamano wakati wa uzinduzi wa baraza hilo tarehe 26 Mei,2023 Jijini Arusha.


Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Naibu Makamu Mkuu Taaluma, Utafiti na Ubunifu Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa. Antony Mshandete ametoa wito kwa wajumbe wa wakilishi wa wafanyakazi katika baraza la wafanyakazi kutumia njia sahihi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Profesa Mshandete ameyasema hayo wakati akifungua na kuendesha mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Arusha.

"Rai yangu kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi ni kubuni njia zitakasaidia katika kuibua bunifu mbalimbali ili kuongeza mapato kupitia rasilimali zinazopatikana katika taasisi yetu" anasema Profesa Mshandete

Anaongeza kwa kueleza kauli mbiu ya chuo chetu ni Taaluma kwa Jamii na viwanda naamini wote tunaisimamia hii katika kuhakikisha tunatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii

Naye Mwakilishi wa Kamishina wa Kazi, Bw. Mussa Msami alisema ushirikiswaji wa wafanyakazi katika mambo yanayoendelea kufanywa na uongozi huleta umoja na hamasa mahala pa kazi hivyo kuchangia kuongeza ari ya ufanyaji kazi.


Aliongeza kwa kuaainisha majukumu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi ikiwemo utendaji kazi, uvumilivu, nidhamu na ubunifu kusaidia uongozi katika utendaji na kusisitiza taasisi itajengwa na watu wenye utu na ari.

Aidha Bw. Mussa ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela kwa kutenga siku maalumu ya uzinduzi wa baraza hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa THTU Taifa Bw. Paul Loisulie amewaasa wajumbe wa baraza hilo kuzingatia utunzaji wa siri za taasisi na kuepuka kutoa au kupokea taarifa kutoka kwenye vyombo visivyo rasmi.

Post a Comment

0 Comments